|
6) KUITADILI BAADA YA RUKUU:
Hii
ndiyo nguzo ya sita katika mlolongo wa nguzo za swala. Na kuitadili
maana yake ni kusimama na kulingana sawa baada ya kuinuka kutoka rukuu.
Kwa hiyo tunaweza kabisa kusema kuwa kuitadili ni kisimamo sawa kinacho
tenganisha baina ya rukuu na sijida.
Dalili ya Itidali: Itidali kama mojawapo ya nguzo za swala imetajwa
katika riwaya iliyo pokelewa kutoka kwa Bi. Aisha-Allah amuwiye
radhi-kwamba yeye aliielezea swala ya Mtume-Rehema na Amani
zimshukie-akasema: “Alikuwa anapo kiinua kichwa chake kutoka rukuu,
husujudu mpaka (kwanza) alingane sawa hali ya kusimama (aitadili)”.
Sharti za Itidali:
Ili Itidali iswihi, kumeshurutizwa mambo yafuatayo:
i. Kutokukusudia kwa kuitadili kutoka rukuu kitu kingine chochote zaidi ya ibada.
ii. Kutulizana katika Itidali kiasi cha kadiri ya kuleta Tasbihi moja.
iii. Asirefushe mno kisimamo cha Itidali kiasi cha kuzidi muda
unaotumika katika usomaji wa Suratil-Faatihah. Hii ni kwa sababu
Itidali ni miongoni mwa nguzo fupi, kwa hivyo basi hakujuzu
kuitwawilisha (kuirefusha).
7) KUSUJUDU MARA MBILI KATIKA SWALA:
Nguzo ya saba ya swala ni kusujudu. Na maana ya sijida ni kugusa paji la uso la mswaliji mahala anapo sujudu.
Dalili ya sijida: Sijida kama nguzo ya swala ni agizo na amri ya Allah
itokanayo na kauli yake tukufu: “ENYI MLIO AMINI! RUKUUNI NA SUJUDUNI
NA MUABUDUNI MOLA WENU NA FANYENI MEMA, ILI MPATE KUFAULU”.2
Na kauli yake Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-alipo mwambia yule
mtu aliye kosea katika swala yake: “...Kisha sujudu mpaka utulizane
hali ya kusujudu. Halafu inuka utulizane hali ya kukaa, halafu sujudu
(tena) mpaka utulizane hali ya kusujudu...”.
Sharti za sijida:
Ili sijida iswihi kisheria, kumeshurutizwa kuchunga mambo yafuatayo:
a) Paji la uso liwe wazi wakati wa kugusana na ardhi.
b) Kusujudu kuwe ni kwa viungo saba alivyo vitaja Bwana Mtume-Rehema na
Amani zimshukie-kupitia kauli yake: “Nimeamrishwa kusujudu kwa
(kutumia) mifupa (viungo) saba; Juu ya paji la uso – na akaashiria kwa
mkono wake pua yake – na mikono na miguu na ncha za (vidole vya)
miguu”.3
Tanbihi: Si wajibu kuacha wazi chochote katika viungo saba hivi vilivyo tajwa ila paji la uso tu.
c) Sehemu yake ya chini (kiuno) iinuke zaidi kuliko ile ya juu (mabega)
kiasi kimkinikacho. Kufanya hivyo ni kufuata kitendo cha Bwana
Mtume-Rehema na Amani zimshukie.
d) Hasisujudu juu ya nguo iliyo ambatana naye inayo tukutika kwa mtukutiko wake, mithili ya kilemba au kashida yake.
e) Hasikusudie kitu kingine chochote zaidi ya sijida, mithili ya kuporomoka kwa ajili ya hofu.
f) Kukandamiza kidogo paji lake katika ardhi kwa sura ambayo kama
ingekuwepo hapo anapo sujudu pamba au kitu mithili ya pamba, ingebonyea
na athari ya sijida kudhihiri hapo.
g) Kutulizana katika sijida kwa kadiri ya kuleta Tasbihi moja.
Na ukamilifu wa sijida ni mswaliji kuleta Takbira ya kuporomokea sijida
na kuweka ardhini magoti yake yakifuatiwa na mikono. Halafu paji na
kumalizia na pua yake na aiweke mikono yake welekeya (mkabala) wa
mabega yake na avitandike vidole vyake kwa kuvikusanya vikiwa
vimeelekezwa Qiblah. Na aliepushe tumbo lake kugusana na mapaja yake,
na dhiraa zake zisigusane na ardhi wala mbavu zake. Na aseme mara tatu:
SUB-HAANA RABBIYAL-A’ALAA. Imepokelewa kutokana na hadithi ya Abu
Hurayra-Allah amuwiye radhi-katika kuielezea swala ya Bwana
Mtume-Rehema na Amani zimshukie: “...Kisha husema: ALLAAHU AKBAR,
wakati aporomokapo hali ya kusujudu...”.4
Na imepokelewa kutoka kwa Abdillah Ibn Maalik Ibn Buhaynah-Allah
amuwiye radhi-kwamba Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-alikuwa
anaposwali, huweka mwanya baina ya mikono yake mpaka unaonekana weupe
wa kwapa zake”.5
Imepokewa kutoka kwa Al-Baraai-Allah amuwiye radhi-amesema: Mtume wa
Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: “Unapo sujudu, basi weka
vitanga vyako (ardhini) na vinyanyue viko (mirfaq) vya mikono yako”.6
Na imepokewa katika kutaja wasifu wa swala ya Bwana Mtume-Rehema na
Amani zimshukie: “...na anapo sujudu, husema katika sijida yake:
SUB-HAANA RABBIYAL-A’ALAA, mara tatu...”.7
Tanbihi: Mwanamke huhitilafiana na mwanaume katika baadhi ya vipengele
tulivyo vitaja. Yeye ataukusanya pamoja mwili wake wakati wa kusujudu.
Imepokelewa kwamba Bwana Mtume-Rehema na Amani zimshukie-aliwapitia
wanawake wawili hali ya kuwa wanaswali, akawaambia: “Mnapo sujudu
(kuelekea ardhini), basi zikusanyeni baadhi ya nyama, kwani mwanamke
siyo kama mwanaume katika hilo”.8
8) KITAKO BAINA YA SIJIDA MBILI:
Kitako hiki baina ya sijida mbili ni wajibu kiwepo katika kila rakaa.
Dalili ya kitako hiki: Kitako hiki kilicho baina ya sijida mbili;
ile ya kwanza na ya pili, kimetajwa katika kauli yake Bwana
Mtume-Rehema na Amani zimshukie-iliyo pita: “...Halafu inuka utulizane
hali ya kukaa...” [Rejea dalili za sijida]
Sharti za kitako baina ya sijida mbili: Kumeshurutizwa katika kuswihi kwa kitako hiki, kuchunga mambo yafuatayo:
Akusudie ibada kwa kitako chake hicho na siyo kingine chochote, mithili ya kukaa kwa sababu ya hofu.
Asikitwawilishe (asikirefushe) sana kitako hicho kiasi cha kuzidi muda wa uchache wa Tashahudi.
Kutulizana kiasi cha kuleta Tasbihi moja.
9.
KIKAO
CHA MWISHO.
Hapa
kinachokusudiiwa ni kile kitako kinachokuwa katika rakaa ya
mwisho ya
swala, kinachofandamiwa na salamu.
Ni
suna iliyothibiti
kukaa mkao wa “ Tawarruki”
katika kikao hiki cha
mwisho . Huu ni
mkao ambao mtu hukalia tako la kushoto
na sehemu
ya tako la kulia , akaunyoosha
mguu wa kulia kama unavyokuuwa katika si
jida na kuupitisha ule wa kushoto chini yake.
Imekuja
kaatika
riwaya ya Abuu
humayd : “ ……………..hata ilipokuwa sijida ambayo ndani yake
ndimo imo salamu ( sijida ya mwisho )
huutoa
mguu wake wa
kushoto na akakaa mkao wa tawarruki kwa kukalia tako lake la kushoto”
Abuu Daawound
10.
TASHAHUDI YA MWISHO { KATIKA KIKAO
CHA MWISHO}
Ni
wajibu kwa mwenye
kuswali akae
baada
ya sijda ya
mwisho ya swala yake asome “Tashahudi”
imepokelewa katika riwaya ya Ibn
Masoud Allah amuwiye radhi – amesema : Tulikuwa tukisema kabla ya
kufaradhishwa juu yetu Tashahudi
ASSALAAM
ALALLAH KABLA IBADIHI, ASSALAAM ALAA JIBRILL, ASSALAAM ALA MIIKAIL, ASSALAAM
ALA FULAN
Mtume
- Rehema na amani zimshukie
alipomalizaa kuswali alituelekkea , akatuambia “ Hakika
Allah ndiye AS – SALAAM , basi anapokaa mmoja wenu
katika
swala { Kwa
ajili ya Tashahudi } basi
na aseme
ATTAHIYYAAT
LILLAH WASSALAWATU WATTAYYIBAATU, ASSALAAM ALAYKA AYYUHA NNABII WARAHMATULLAH
WABARAKATUH, ASSALAAM ALAYNA WA-ALAIBADILLAHI SSALIHINA
Kwani
nyinyi mtakapoisema {salamu
hii}
humpata {humfikia} kila mja mwema mbinguni na ardhini.
Bukhaari na
Muslim.
Hili
ni mojawapo ya matamko
sahihi ya
Tashahudi ambayo
yaliyonukuliwa kutoka kwa Bwana
Mtume. Tashahudi yeyote iliyothibiti kutoka kwa Mtume mtu
akiisoma itamjuzia.
Sharti
za Tashahudi.
Msomaji
wa Tashahudi analazimika kuchunga yafuatayo:
-
Ajisikizishe
yeye
mwenyewe matamko ya Tashahudi
iwapo hana tatizo la kusikia.
-
Kukifululiza
kisomo cha tashahudi, yaani asiweke mwanya mkubwa baina ya ibara za
Tashahudi . pia asitie kati dhikri nyingine , akifanya hivyo yaani
akinyamaza kinyamao kirefu au
akilia kati dhikhri
nyingine , Tashhahudi yake
itakuwaa imebatilika na itamuwajibikia kuianza upya.
-
Aisome
katika hali ya kukaa isipokuwa katika mazingira ya dharura tu ndio
anaruhusiwa kuisoma
katika hali
yoyote imkinikiayo.
-
Aisome
kwa lugha ya
Kiarabu . Akishindwa atasoma tafsiri yake kwa Lugha
yake, Lakini bado atakuwa na wajibu wakujifunza mpaka aweze kuisoma
kiarabu kama alivyofanya Mtume wa Allah- Rehema na Amani zimfikie.
-
Achunge
matokeo ya herufi , shada na hukumu zote za usomaji . akifanya kosa
lolote litakalopelekea
kuharibika
kwa maana,
halitamaanisha zaidi ya
kubahatilika Tashahudi yake
hiyo . Kwa
hivyo basi itamlazimu kuirejea upya .
-
Ayatungamanishhe
maneno ya Tashahudi
kwa mtungo wake kama yalivyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allah –
Rehema na Amani
zimshukie .
|