|
Hizi ni
aina ya suna za swala ambazo huletea baada ya swala kumalizika. Hizi
zinakusanya:-
1.
Kuleta Istighfaari, dhikri na dua.
Imepokelewa
kwamba Mtume Rehama na Amani zimshukie alikuwa anapomaliza swala yake
huleta Istingfaari mara tatu na kisha akasema.
ALLAHUMMA
ANTASSALAAM, WA MINKASSALAAM, TABAARAKTA YAA DHALJALAAL WAL-IKRAAM
Muslim
Si
vibaya kunyanyua sauti kwa Imamu wakati wa kuleta Istighfaari, dhikri na
dua, kwa lengo la kuwafundisha maamuma wake. Wakishajua na kuzoea hasi
walete dhikri hizo kwa sauti ya chini, isiyo ya kusikika kiasi cha kuwa ni
kishawishi kwa watu wengine wanaoswali.
Imepokelewa
kutoka kwa Ibn Abbaas Allah awawiye radhi kwamba kunyanyua sauti kwa
dhikri wakati watu wanapomaliza swala ya fardhi, kulikuwepo zama za Mtume
– Rehema na Amani zimshukie.
Bukhaariy
na Muslim.
Imepokelewa
kutoka kwa Ka’ab Ibn Ujirah – Allah amuwiye radhi kwamba Mtume Rehema
na Amani zimshukie amesema “Viandamizi, harejei patupu msemaji wake
baada ya kila swala ya faradhi (Viandamizi hivyo ni) Tasbih
(Sub-haanallaah) thelathini na tatu, Tahmiydah (Al-hamdulillaah)
thelathini na tatu, na Takbiyrah (Allaahu Akbar) thelathini na tatu”
Muslim
Imepokelewa
kutoka kwa Muaadh Ibn Jabal – Allah amuwiye radhi – kwamba Mtume wa
Allah – Rehema na Amani zimshukie alimshika mkono wake na kusema: “Ewe
Muaadh, Wallah hakika mimi ninakupenda, akasema: “Ninakuusia ewe Muaadh,
usiache usiache baada ya kila swala kusema:
ALLAHUMMA
A’INNI ALAA DHIKRIKA WA SHUKRIKA WAHUSNI IBAADATIKA
Abuu
Daawoud
Zipo
dua na adhkaari nyingi sana za baada ya swala zilizopokewa kutoka kwa
Bwana Mtume, unaweza kurejea vitabu vya hadithi na Adhkaari ikiwa unapenda
kuzijua.
2.
Kugura kwa ajili ya swala ya suna kutoka mahala
paliposwaliwa swala ya fardhi.
Ni
suna iliyothibiti kutoka kwa Bwana Mtume, mtu kugura (kuhama) mahala
aliposwalia swala ya fardhi kwa ajili ya kuswali
swala ya suna baada ya swala mahala pengine Falsafa ya suna hii ni
kwamba mahala anaposujudu mja patamshuhudia mbele ya Allah, kuitekeleza
suna hii hakutamaanisha kingine zaidi ya kukithiri kwa sehemu
zitakazomshuhudia (zitakazomtolea ushahidi).
Lakini
ni bora zaidi kama hakuna kipingamizi (dharura) kwenda kuswali swala ya
suna
nyumbani kwake mtu baada ya kuiswali swala ya faradhi msikitini
pamoja na jamaa. Hayo ndiyo maelekezo na mafundisho kutoka kwa Bwana Mtume
– Rehema na Amani zimshukie:
“Enyi watu, swalini
majumbani mwenu, kwani bora ya swala ni mtu
kuswali nyumbani kweke ila swala ya fardhi”
Bukhaariy na Muslim.
Xi
NAMNA YA KUSWALI
Baada
ya kujifunza mambo mengi yahusianayo na swala, sasa ni vema tukajifunza
namna ya kuswali ili kulitekeleza agizo la Mtume wa Alalh – Rehema na
Amani zimshukie – lisemalo:
“Swalini
kama mlivyoniona mimi nikiswali Bukhaariy.
Ni
dhahiri kwamba amri na maelekezo haya ya
Bwana Mtume yalikuwa yanawagusa moja kwa moja maswahaba wake, kwa
kuwa wao ndio walikuwa pamoja nae wakamuona anavyoswali. Ama sisi amri
hiyo nasi inatugusa lakini si kwa njia ya moja kwa moja kama maswahaba.
Sisi hatuwezi kuswali kama alivyoswali Bwana Mtume kwa kuwa hatukuishi nae
kwa hiyo hatukupata bahati ya kumuona akiswali kama alivyofundishwa na
mwalimu wake Malaika Jibril-Amani ya Allah imshukie kwa amri na maelekezo
ya Allah: “Alinijia Jibril – Amani imshukie mwanzo kabisa mwa wahyi
(ufunuo) akanifundisha udhu
na swala………………..”
Al-haakim, Baihaqiy na Ahmad.
Sisi
tunaswali kama maswahaba wa Mtume wa Allah – Allah awawiye radhi, kwani
wao ndio waliotufundisha dini ndani yake ikiwemo swala. Ni kwa kuwafuata
wao tu ndio tunaweza kuswali kuwa alivyoswali Mtume
wa Allah. Sasa hebu tufuatane nao kwa makini watufundishe swala ili nasi
tuweze kuswali kama alivyokuwa akiswali mwenyewe Bwana Mtume, nae kama
alivyofundishwa na Jibril kwa amri ya Allah. Ewe Mola wa haki wee!
Tuongoze na utuwafikishe kuswali, kufunga, kuhiji, kutoa zakkah na baki ya
amali nyingine kama alivyofundisha kipenzi chako, Nabu Muhamaad Aamiyn!
Haya
na tuswali sasa:
1.
Baada ya kujitwaharisha na kuingia wakati wa
swala unayotaka kuiswali na kujistiri tupu (uchi) kama tulivyobainisha
katika darasa zilizotangulia, simama wima uelekee Qiblah kwa kuitekeleza
amri ya Mola wako. “NA POPOTE UENDAKO GEUZA USO WAKO KWENYE MSIKITI
MTAKATIFU.NA POPOTE MLIPO GEUZENI NYUSO ZENU UPANDE ULIKO (msikiti
huo)……………………. (2: 150)
Muradi
na makusudio ya “msikiti Mtakatifu” hapa ni dhati ya Al-ka’abah”,
hivi ndivyo inavyobainishwa na hadhiti kadhaa. Miongoni mwazo ni hii:
Imepokelewa
na Ibn Abbaas – Allah awawiye radhi amesema: Mtume Rehama na Amani
zimshukie alipoingia ndani ya Al-ka’abah aliomba dua katika pande zake
zote na hakuswali (mle ndani) mpaka alipotoka nje. Alipotokea nje akaswali
rakaa mbili mbele ya Al-kaabah na akasema “Hiki ndio Qiblah. Bukhaariy
na Muslim.
2.
Baada ya kusimama na kuelekea Qiblah, ni wajibu
utie nia ya swala unayotaka kuswali moyoni. Huko ni kumfuata Mtume kwa
kutekeleza kauli yake, “Hakika si vinginevyo amali zote zimefungamaan na
nia na kila mtu atalipwa kwa kadri ya nia yake………”
Bukhaariy
Nyanyua
vitanga vya mikono mpaka mkabala wa mabega yako hali ya kuleta nia na
kisha useme (Allah Akbar) Hivyo ndivyo ilivyopokelewa kutoka kwa Ibn Umar
– Allah awawiye radhi – amesema: “Alikuwa Mtume wa Allah Rehema na
Amani zimshukie anaposimama kuswali, hunyanyua mikono yake (vitanga) mpaka
ikawa mkabala na mabega yake kisha akakabiri (akasema Allahu
Akbar)………..”Muslim.
3.
Halafu funga swala kwa kuiteremsha mikono na
kuiweka chini ya kifua, huku ukiushika mgongo wa kitanga cha mkono wa
kushoto kwa kile cha kulia. Hivi ndivyo atufundishavyo swahaba Waail Ibn
Hijri – Allah amuwiye radhi amesema: “Nilimuona Mtume wa Allah –
Rehema na Amani zimshukie anapoingia ndani ya swala
huushika mkono wake wa kushoto kwa ule wa kulia’ Ibn Mundhir, Ibn
Khuzaymah na Abuu Dawoud.
4.
Kisha fungua swala yako kwa kuleta dua ya
ufunguzi wa swala (Iftilaahi). Hili linatokana na kauli ya Imam Aliy-Allah
amuwiye radhi amesema: “Alikuwa Mtume wa Allah- anaposimama kuswali
husema.
WAJJAHTU
WAJHIYA LILLADHI FATARASWAMAAWATI WAL-ARDHI HANIIFAN WAMAA ANA
MINALMUSHRIKIIN, INNA SWALAATIY WA NUSUKII WA MAHYAAYA WA MAMAATIY LILLAHI
RABBIL-AALAMIIN LAA SHARIIKA LAHU WABIDHALIKA UMIRTU WA ANAA
MINAL-MUSLIMIIN. Muslim na Ibn Hibban.
5.
Baada ya kumaliza kusoma dua hiyo ya ufunguzi wa
swala, lete “Audhubillah kabla ya kuanza kusoma Al-hamdu. Hayo ndiyo
maelekezo ya Mola wako, sikia: “NA UKITAKA KUSOMA QUR-ANI PIGA AUDHU
(Kwanza, jikinge) KWA ALLAH (akulinde) NA SHETANI ALIYEFUKUZWA (Katika
rehema ya Allah)” (16: 98)
Kadhalika
imepokelewa kutoka kwa Mtume – Rehema na Amani zimshukie kamba:
“Alikuwa akisema baada ya Iftitaahi (dua ya ufunguzi) na kabla ya kisomo
(cha Al-hamdu).
AUDHU
BILLAHI-SSAMI’UL-ALIIM MINAS-SHAITAANI-RRAJIIM. Abuu Daawoud.
6.
Halafu soma Suuratil – Faatihah (Al-hamdu) kwa
kuanza na Bismillahi kwani hiyo Bismillahi ni aya miongoni mwa aya zake
(Al-hamdu). Hivyo ndivyo ilivyopokelewa kutoka kwa Abuu Huray-rah-Allah
amuwiye radhi – amesema: Amesema Mtume wa Allah – Rehema na Amani
zimshukie: “ Mnaposoma Al-hamdulillah” someni
BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM kwani hiyo ndiyo Umul-Qur-ani, Umul-Kitaab na
Sab-ul-mathaaniy, na BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
ni mojawapo ya aya zake. Daaru qutwniy na Baihaqiy.
7.
Unapofikia
mwisho wa Al-hamdu WALADHWAAALIIN itikia “Amiyn” Hivi ndivyo
ilivyopokelewa na Abuu Hurayrah – Allah amuwiye radhi – kwamba Mtume
wa Allah – rehema na Amani zimshukie amesema: “Atakaposema
Imamu WALADHWAAALIIN Semeni Aamiyn, kwani itakayewafikiana Aamiyna
yake na Aamiyna ya malaika, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia
(yaliyopita)”
Bukhaairy.
|