|
Mtu mwenye kuacha swala ama
Taarikuswalaat kama anavyojulikana katika sheria.
Huyu ama atakuwa ameiacha swala kwa uvivu
tu na uzembe au atakuwa ameiacha kwa kuipinga
kuwa si wajibu na kuiona kuwa si cho chote.
Hukumu ya
mtu huyu kisheria inaiandamia sababu ya kuacha
kwake swala. Kwa mantiki hii mtu mwenye kuacha
swala kwa kupinga na kukanusha uwajibu wa swala
kwake au kwa kuifanyia shere. Huyu kwa upingaji
wake huu ana kuwa ni KAFIRI na ANATOKA KATIKA
UISLAMU. Sheria inamuwajibisha kiongozi kumuamrisha muacha swala huyu
kutubia, akikubali kutubia baada ya kutakwa toba
na akasimamisha swala itakiwavyo. Atarejea kuwa
muislamu na hivyo kupata kinga ya nafsi na mali
yake, yaani itakuwa si halali kuuliwa. Kama
hakukubali kutubia, kiongozi ataamuru kuuliwa na
atauliwa hali ya kuwa ni murtadi (ametoka
katika Uislamu). Baada ya kuuawa si jaizi
kukoshwa, kukafiniwa (kuvikwa sanda) wala
kumswalia.
Kama isivyojuzu kumzika katika makaburi
ya waislamu kwa sababu yeye si miongoni mwa
waislamu.
Ama
mtu akiiacha swala kwa uvivu tu huku akiitakidi
kuwa ni wajibu kwake.
Huyu atakalifishwa kuikidhi swala
aliyoiacha na kutubia kutokana na maasi ya
kuacha swala mbele ya kiongozi.
Kama hakuinuka kutekeleza amri ya
kiongozi ya kukidhi swala, atauwawa kwa
“haddi” (penalty). Yaani kutazingatiwa
kuuawa kwake ni kutiwa adabu kwa mujibu wa
sheria kama wanavyotiwa adabu maasi wengine (mzinifu,
mwizi na kadhalika). Huyu atazingatiwa kuwa ni
muislamu baada ya kuuawa, kwa hivyo atatendewa
yote wana yotendewa waislamu. Ataoshwa,
atakafiniwa, ataswaliwa na kuzikwa katika
makaburi ya waislamu kwa sababu ni mmoja wao.
Imepokelewa
kutoka kwa Ibn Umar–Allah awawiye radhi–kwamba
Mtume wa Allah–Rehema na Amani zimshukie–amesema:
“Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka
Washuhudie kwamba hapana apasaye/afaaye
kuabudiwa kwa haki ila Allah, na washuhudie kuwa
Muhammad ni Mtume wa Allah. Na wasimamishe swala,
na watoe Zakah. Wakiyatekeleza hayo watakuwa
wamezihifadhi kwangu damu zao na mali zao ila
kwa haki ya Uislamu na hisabu yao ni juu ya Allah”.
Bukhaariy & Muslim
Hadithi
hii inafahamisha kwamba mtu aliyekiri na kutamka
shahada mbili atapigwa/atauwawa kama
hakusimamisha swala na wala hawi kafiri.
Dalili na ushahidi wa hili ni ile riwaya
iliyopokelewa kutoka kwa Ubaadah Ibn As-swamit–Allah
amuwiye radhi–amesema: Nilimsikia Mtume wa
Allah–Rhema na Amani zimshukie–akisema:
“Swala tano amezifaradhisha Allah kwa waja
wake, atakayezitekeleza bila ya kupoteza cho
chote katika
hizo swala kwa sababu ya kuikhafifisha
haki yake. (Huyu) atakuwa na ahadi mbele ya
Allah ya kumuingiza peponi.
Na asiyezitekeleza, hatakuwa na ahadi
mbele ya Allah, akitaka atamuadhibu (kwa kuacha
kwake swala) na akitaka atamuingiza peponi”. Abuu Daawoud & wengineo.
Hadithi hii pia inafahamisha kuwa muacha
swala hawi kafiri, kwa sababu kama angelikuwa
kafiri asingeliingia katika kauli ya Mtume:
“...na akitaka atamuingiza peponi.”
Kwa maana kafiri haingii katu peponi, kwa hivyo
ikachukuliwa kuwa huyu ni yule aliyeiacha swala
kwa uvivu. Hili linatokana na mjumuisho wa
dalili.
Imepokelewa
hadithi kutoka kwa Jaabir–Allah amuwiye radhi–
amesema: Nilimsikia Mtume-Rehema na Amani
zimshukie–akisema: “Hakika baina ya mtu na
shirki na ukafiri ni kuacha swala.” Muslim
& wengineo.
Hadithi
hii inachukuliwa juu ya kuacha swala kwa kupinga
ufaradhi wake na kuikanusha au kuicheza shere na
kuiona kuwa si cho chote.
|