|
UISLAMU.
01.
DINI
Kila
sikio la mwanadamu aliyewahi kuishi, anayeishi
na atakayekuja kuishi katika ulimwengu huu
limepata kulisikia, linasikia na litalisikia
neno “dini” Neno hili “dini” neno fupi
Kabisa, neno lenye herufi nne tu, d+i+n+I ni
neon hai au tunaweza kusema ni neno linalobeba
dhana hai iishiyo sambamba na mwanadamu. Ni
sawasawa mwanadamu analitambua hilo au
halitambui au anajitia kutokulitambua, kwani
kule kutokuitambua kwake hakuondoshi/hakufuti
ukweli kuwa yeye na dini ni washirika pacha
katika maisha haya. Kwa hiyo basi neno hilo
fupi na jepesi mno kutamka ulimini “dini”
lina athari kubwa katika maisha ya kila siku
ya mwanadamu na ulimwengu wake kwa ujumla.
Athari hiyo inaweza ama kuwa nzuri au mbaya
kutegemeana na ufahamu/uelewa wa mwanadamu
kuelekea dhana hii dini.
01:01-
MAANA YA DINI:
Wanadamu
kama viumbe waliotofautiana katika maumbile (sura),
lugha, rangi, hali za kimaisha, fikra na
kadhalika. Wameielewa “dhana dini” kwa
maana mbalimbali. Maana hizi ukizingatia kwa
fikra za haraka haraka, fikra za kijuu juu
zisizochimba na kupenya ndani. Utaona kuwa
zinatofautiana, lakini ukweli na hakika ni
kwamba zinaona na kuhusiana kwa namna moja au
nyingine hii ni kwa sababu zote zinachimbuka
kutoka katika chemchem moja ambayo ni akili ya
mwanadamu. Sasa basi ukizijumuisha na
kuziunganisha pamoja maana hizo, hatimaye
utatoka na natija ya mwisho kwamba kumbe dini
kama aielewayo mwanadamu ni:
(Mfumo/utaratibu
Fulani wa maisha unaofuatwa na jamii Fulani ya
wanadamu).
Hili
ndilo eleweko la dhana dini kupitia akili,
fikra na mawazo ya binadamu. Sasa basi ili
kuutambulisha kwa walimwengu mfumo wa maisha
aufuatao mwanadamu akaamua kuupa jina mfumo
wake huo aliojichagulia na kuufuata. Unaweza
kuukuta mfumo huo chini ya majina kama
mila/desturi/utamaduni, au ujamaa,
ukomunisti, ubepari, kutoamini kuwepo kwa
Munguu (Atheism), ushirikina (Polytheism) na
kadhalika. Hii yote ni miongoni mwa mifumo hai
ya maisha inayofutawa na matabaka Fulani ya
watu wanaounda jamii ya wanadamu katika
ulimwengu huu.
01:02-
HISTORIA YA DINI:
Baada
ya kuiangalia kwa mukhtasari dhana na maana ya
dini, hebu sasa tujiulize dini imeanzia wapi?
Tukiichukulia dini kwa maana ya aina Fulani ya
mfumo wa maisha uliochaguliwa na kufuatawa na
Jamii Fulani ya wanadamu. Tutagundua kwamba
historia ya dini inaenda sambasamba na
historia ya kuanza kuwepo kwa mwanadamu katika
maisha ya ulimwengu huu. Hili ni dhahiri kwa
sababu hakuna mwanadamu aliyepata kuishi,
anayeishi au atakayeishi katika ulimwengu huu
bila ya kufuata mfumo maalumu wa maisha. Iwe
ni mfumo alio na khiyari nao mithili ya hizo
mila/desturi, ujamaa, ubepari, ukomunisti na
kadhalika. Au ule asio na khiyari nao mithili
ya ule utaratibu mzima wa tangu kutungana kwa
mimba, kuzaliwa mpaka kufa na yote
yahitajikayo ili kuukamilisha utaratibu huu.
Kwa mantiki hii basi huu unakuwa ni ushahidi
wa kimazingira unaoonyesha kuwa dhana dini
imeanza kuishi sambasamba na mwanzo wa kuwepo
kwa mwanadamu katika ulimwengu huu.
01:03-
KWA NINI DINI? (UMUHIMU WA DINI KATIKA MAISHA
YA MWANADAMU)
Ingawa
katika ulimwengu huu tuishimo kuna watu
wanaoutaka ulimwengu uelewe kuwa mahitaji
makuu ya msingi ya mwandamu ni maskani (nyumba),
mavazi na chakula. Yaani ili mwanadamu aweze
kuishi katika ulimwengu huu ni lazima apate
vitu hivi. Ni sawa kwa kiwango Fulani kusema
hivi lakini hili halizuii ukweli kwamba
mwanadamu anaweza kuishi kwa muda Fulani bila
ya vitu hivi vyote. Hata hivyo mwanadamu hana
namna ya kuepa kuishi bila ya kufuata dini
yeyote japo kwa sehemu ya sekunde. Ukweli huu
unatokana na dhana hai kwamba hakuna mwanadamu
anayeishi bila ya kufuata mfumo fulani wa
maisha. Uwe mfumo huo ni ule uliobuniwa na
wanadamu wenyewe kwa ajili ya jamii Fulani (mfumo
binadamu). Au ni ule aliochaguliwa mwanadamu
na Mungu Muumba wake. Kwa hivyo, tutaona
kwamba mwanadamu ni kiumbe mwenye maumbile
yanayomlazimisha kufuata mfumo fulani katika
kuyaendea maisha yake ya kibinafsi sambamba na
yale ya kijamii. Kwa mantiki hii hatuna namna
ya kuepa kusema kuwa mwanadamu hawezi kuishi
bilaya dini, bila ya kujali usahihi au ubatili
wa dini hiyo.
01:04
– NI MFUMO GANI KHASA WA MAISHA (DINI) ANAOUHITAJIA
MWANADAMU?
Tumekuishaona
kwamba dini ni mfumo Fulani wa maisha
unaofuatwa na binadamu. Sasa suala
linalojitokeza ni je, ni mfumo upi wa maisha (dini)
unaomfaa mwanadamu? Tuanze kulijibu swali hili
kwa kuanza kusema kwamba tangu zama za kale
mwandamu amekuwa katika harakati za kupigania
kupata maisha ya furaha na amani. Si hivi tu
bali pia kuunda jamii adilifu. Harakati hizi
zinaaathiriwa kwa kiwango kikubwa na itikadi
au mfumo maisha unaofuatwa na jamii husika.
Mfumo
sahihi wa maisha au dini ya kweli inayomfaa
mwanadamu na itakayokidhi kiu ya mwanadamu
katika kupata maisha ya amani na furaha, ni
lazima iwe:-
-
Inalingana/inayokubaliana
na maumbile ya mwanadamu na ulimwengu
aishimo.
-
Na
itikadi inayokubali kuhojiwa na kuingia
akilini.
-
Inakidhi
mahitaji asili ya kimaumbile ya mwanadamu
kiroho na kimwili.
-
Inaweza
kujibu maswali ya mwanadamu kuhusiana na
uumbwaji huu wa ulimwengu sambamba na yeye
mwenyewe.
-
Inaweza
kumuonyesha mwanadamu nafasi lengo na
wajibu wake katika maisha haya.
-
Na
uwezo wa kukidhi mahitaji ya kiakili,
kimaono na kihaiba ya mwanadamu.
-
Ni
dini ya ulimwengu mzima kwa ajili ya
walimwengu wote kwa zama zote.
Kwa
kuzingatia nukta hizi kama kigezo/mizania ya
dini/mfumo sahihi wa maisha unaomfaa mwanadamu.
Tutaona kuwa hakuna mfumo unaoweza kuzigusa
nukta zote hizi kwa ukamilifu zaidi ya ule
Allah Mola Muumba aliowachagulia mwanadamu. Na
huu si mwingine bali ni mfumo Islamu.
02.
UISLAMU.
Uislamu
ndio dini ya maumbile bila ya makindano. Yaani
Uislamu ndio mfumo wa maisha unaokwenda
sambamba na maumbile ya mwanadamu na ulimwengu
wake. Kwa mantiki hii tunaweza kusema kwa
kinywa kipana kabisa kwamba Uislamu ndio dini
ya jamii ya wanadamu. Uislamu haukuitwa dini
ya jamii ya wanadamu kwa kuropoka tu au kwa
hamasa na jazba. Imeitwa hivyo kwa sababu
zifuatazo:-
-
Imesheheni
desturi zinazokubaliana na akili.
-
Ina
uongofu unaouangazia na kuupa nuru moyo.
-
Inabeba
maendeleo yanayofaa kwa hali, mahala na
zama zote.
-
Ina
sheria inayokidhi hali na mahitaji yote ya
jamii katika nyanja zote za maisha.
-
Ina
dhana ya usawa unaowaunganisha pamoja watu
wote bila ya kujali lugha, rangi au hali
zao za kimaisha.
-
Sheria
yake ina dhima ya kumpa mwanadamu maisha
ya amani, utulivu, raha, furaha na heshima
katika nafsi, mwili, akili na mali.
Haya
na mengineyo ndiyo yanayoufanya Uislamu uwe ni
dini inayokubaliwa na kuridhiwa na mwanadamu
kwa kuwa inayogusa moja kwa moja maumbile yake.
02:01
– UISLAMU NI NINI?
Uislamu
ni mfumo kamili na sahihi wa maisha unaozienea
nyanja zote za maisha ya mwanadamu katika hali,
mahala na zama zote. Mfumo uliofumwa na Allah
Mola Muumba ulimwengu na walimwengu kwa ajili
ya waja wake na akawaleta kupitia mitume wake.
Tangu Nabii Adamu mwanadamu wa kwanza mpaka
Nabii Muhamad Mtume wa mwisho. Ili uwe ni
muongozo na katiba ya kukiendesha kila
kipengele cha maisha yao katika maisha haya ya
mpito ya ulimwengu huu yenye dhima ya
kuwaandaa na maisha ya milele ya Akhera.
02:02
– KAULI MBIU YA UISLAMU.
Uislamu
kama dini na mfumo sahihi na kamili wa maisha
unalingana na kuhubiri juu ya kuwepo Mungu
aliye Muumba wa mbingu na ardhi na vyote
vilivyomo humo. Unawataka wanadamu wote
waitakidi kuwa YEYE ni MUNGU MMOJA WA PEKEE
ASIYE NA MSHIRIKA YEYE tu ndiye anayestahiki
kukusudiwa na
viumbe wake wote kwa kumuabudu,
kumuomba na kumtegemea. YEYE hakuzaa wala
hakuzaliwa wala YEYE hana anayefanana naye
hata mmoja. Hii ndio kauli mbiu ya Uislamu,
dini ya jamii ya wanadamu.
Na
akili isiyo lemavu haiwezi kupinga au
kukanusha kuwepo kwa Mola Muumba wa ulimwengu
na walimwengu kwani kanuni huru za kiakili
zinasema kuwa (kila natija/matokeo yana sababu
yake). Kwa kuichukua kanuni hii yenye mantiki
kama mizani akili haitasita kukubali kuwa kila
kiumbe kina Muumba. Kwa sababu kiumbe ni
natija/matokeo yanayohitaji sababu na sababu
hiyo ndiyo Muumba Mwenyewe. Maadam akili
imetumika kumjua Muumba Mkuu, basi uadilifu wa
kiakili unamsukuma mwanadamu kumuamini.
Kauli
mbiu ya Uislamu inawafikia walimwengu kupitia
ujumbe wa Allah Mola Muumba unaofikishwa kwao
kwa njia ya Mjumbe (Mtume).
ALLAH (MOLA MUUMBA)
UJUMBE (Vitabu)
MJUMBE (Mtume)
WALENGWA
WA UJUMBE (Jamii ya wanadamu).
Huu
ndio utaratibu kamili wa mawasiliano baiana ya
Allah Mola Muumba na mwanadamu kiumbe muumbwa
chini ya mfumo Islamu.
Uislamu
ni AKIDA/ITIKADI na SHERIA
a.
AKIDA:
Ni ile Imani ya kumuamini Allah kuwa ni
Mungu Mmoja Muumba ulimwengu asiye na Mshirika.
Na kumuamini Muhammad kuwa ni Mtume wake kwa
watu wote na kuwaamini Mitume wake kwa watu
wote waliomtangulia katika kufikisha ujumbe wa
Mola wake kwa nyumati zilizoutanguila umati
huu wake. Akida pia inahusisha
kuiamini:-
-
Siku ya mwisho.
-
Kusimamisha swala
-
Kutoa zaka
-
Kufunga Ramadhani
-
Kuhiji Makah.
Mambo
yote haya kwa ujumla wake ndio nguzo madhubuti
na imara zinazolibeba jengo Uislamu. Akida hii
ya UISLAMU ni ndugu baba moja mama mmoja na
akida za mbinguni zilizotangulia kabla yake.
Ambazo zote zina dhima ya kulingania kheri (wema)
na kukemea mambo maovu na machafu. Uislamu
umekuja kuikamilisha dhima hii. Hii ndio AKIDA
ya Uislamu kupitia kitabu cha Uislamu (Qur-ani
Tukufu).
“MTUME
AMEAMINI YALIYOTEREMSHWA KWAKE KUTOKA KWA MOLA
WAKE NA WAISLAMU (Pia wameamini hayo). WOTE
WAMEMUAMINI ALLAH, NA MALAIKA WAKE, NA VITABU
VYAKE, NA MITUME YAKE (nao husema) HATUBAGUI
BAINA YA YOYOTE KATIKA MITUME YAKE (wote
tunawaamini)………..” (2:285)
Na
Uislamu haumlazimishi mtu kuifuata Akida yake
hii kwa nguvu bali aingie Uislamu baada ya
kukinaishwa na hoja zake. Hivi ndivyo
tunavyosema katika kitabu cha Uislamu:
“WAITE (watu) KATIKA NJIA YA MOLA KWAKO KWA
HEKIMA NA MAUIDHA (nasaha) MEMA NA UJADILIANE
NAO KWA NAMNA ILIYO BORA………..”
(16:125)
“HAKUNA
KULAZIMISHWA (mtu kuingia) KATIKA DINI.
UONGOFU UMEKWISHA PAMBANUKA NA UPOTOFU………..”
(2:256) Isitoshe Uislamu unawafundisha
waislamu namna ya kujadiliana na watu wa dini
nyingine.
“WALA
MSIJADILIANE NA WATU WALIOPEWA KITABU (kabla
yenu) ILA KWA YALE (majadiliano) YALIYO MAZURI……….”
(29: 46)
b./ SHERIA
Sheria
ya kiislamu ni mkusanyiko wa maneno ya Allah
Mola Mwenyezi (sheria mama) na maneno ya Mtume
wake kama sheria shereheshi/fafanuzi. Sheria
hii imezienea nyanja zote za maisha ya
mwanadamu kuanzia yale ya kibinafsi mpaka ya
kijamii. Inagusa matendeano ya kila siku baina
ya watu, mahusiano ya watu wenyewe kwa wenyewe,
watu wa viumbe wengine, watu na ulimwenguu wao
na watu na Mola Muumba wao. Kama inavyogusa
mfumo wa familia, mirathi, ndoa, mazishi na
kadhalika.
02:03
– NIKITAKA KUWA MUISLAMU NIFANYE NINI?
Uislamu
unaamini kwamba kila mtoto anazaliwa hali ya
kuwa tayari ni muislamu tokea tumboni mwa mama
yake. Anabakia na Uislamu wake huo wa kuzaliwa
mpaka anapofikia umri wa utu uzima (baleghe)
hali ya kuwa na akili timamu. Katika umri huu
ndipo anapoweza kuitumia akili na khiyari
aliyopewa na Mola wake:
“………….
BASI ANAYETAKA NA AAMINI (awe muislamu) NA
ANAYETAKA NA AKUFURU (awe kafiri). HAKIKA
TUMEWAANDALIA MADHALIMU (Makafiri) MOTO AMBAO
KUTA ZAKE ZITAWAZUNGUKA …………” (18:
29).
Akaukana
na kuuvua Uislamu ndio umbile aliloumbiwa:
“BASI UELEKEZE USO WAKO KATIKA DINI ILIYO
SAWA SAWA NDILO UMBILE ALLAH ALILOWAUMBIA WATU
(yaani dini hii ya kiislamu inawafikiana
barabara na umbo la binadamu). HAKUNA
MABADILIKO KATIKA MAUMBILE YA VIUMBE VYA
ALLAH. HIYO NDIYO DINI ILIYO YA HAKI, LAKINI
WATU WENGI HAWAJUI” (30:30)
Kwa
kufuata mfumo mwingine wa maisha (dini) ulio
nje ya Uislamu ambapo atakuwa amejitia
khasarani mwenyewe: “NA ANAYETAKA DINI
ISIYOKUWA YA KIISLAMU BASI HAITAKUBALIWA KWAKE
NAYE AKHERA ATAKUWA KATIKA WENYE KHASARA (kubwa
kabisa)” (3:85).
Sasa
muasi huyu anapotaka baada ya kuamua kwa
khiyari yake kurudi katika umbile lake la
asili (Uislamu) hahitaji kubatizwa. Kitu pekee
anachotakwia kufanya ni kutamka hadharani
shahada mbili na kuishi kwa mujibu wa shahada
mbili hizo.
02:04
– SHAHADA MBILI NI NINI?
Shahada mbili ni mkusanyiko wa matamko
mawili ya ahadi anayoichukua kiumbe (mwanadamu)
mbele ya Muumba wake na viumbe wenzake. Ambapo
mtamkaji hula kiapo cha utii kwa Allah Mola
Mwenyezi na Mtume wake katika maisha yake yote
kwa kufuata maamrisho na makatazo yake.
1.
SHAHADA YA KWANZA – TAMKO LA UTII KWA
ALLAH:
Ni mtu kutamka kwa moyo na ulimi:-
“ASH – HADU AN LAA ILAAHA
ILLAL-LAAHU”
Maana
: “Ninakiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi
kwamba hapana
afaaye kuabudiwa kwa haki ila
Allah (Mola asiye na mshirika wala
mwana)”
2.
SHAHADA YA PILI: TAMKO LA UTII KWA
MTUME WA ALLAH.
Ni mtu kutamka kwa moyo na ulimi:-
“WA ASH-HADU ANNA MUHAMMADAN ABDUHU
WA RASUULUHU”
Maana:
“Na ninakiri kwa moyo natamka kwa ulimi
kwamba Muhammad ni mja na mjumbe wa Allah (kama
alivyo Isa, Musa, Ibrahimu) Matamko mawili
haya ya ahadi ndio tiketi ya kuingilia katika
Uislamu baada ya mtu kujitoa mwenyewe. Mtu
akiyatamka maneno haya tu tayari anakuwa
muislamu tena na papo hapo anawajibika kuishi
chini ya kivuli na mipaka ya shahada mbili
hizo. Kwani kuishi kwa mujibu wa shahada mbili
ndiko kutampa sifa ya kuwa muumini mbele ya
Alah Mola Muumba wake na mbele ya viumbe (waumini)
wenzake.
02:05
– NGUZO Z A DINI YA KIISLAMU.
Dini
hii ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo tatu za
msingi, ambazo ni:-
1.
UISLAMU, ambao huu umejengwa juu ya
nguzo
tano kama zifuatavyo:-
-
Shahada
mbili
-
Kusimamisha
swala tano
-
Kutoa
zakah
-
Saumu
ya Ramadhani
-
Kuhiji
Makah (kwa mwenye uwezo).
2.
IMANI nguzo hii ya pili ya dini ya Kiislamu inajengeka juu ya nguzo sita
zifuatazo:-
-
Kumuamini
Allah
-
Kuwaamini
malaika wa Allah.
-
Kuviamini
vitabu vya Allah.
-
Kuwaamini
mitume (wote ) wa Allah.
-
Kuamini
siku ya mwisho.
-
Kuamini
qadari ya Allah (ya kheri au ya shari)
kuwa inatoka kwa Allah).
3.
IHSANI. Nguzo hii ya tatu inaundwa na
nguzo hii:-
Kumuabudu
Allah kama unamuona Kama humuoni yeye anakuona
wewe.
Huu
kwa muhtasari ndio Uislamu, dini na mfumo
sahihi na kamili wa maisha kwa wanadamu wote
waliochaguliwa na Allah Mola Muumba wao:
|………LEO NIMEKUKAMILISHENI DINI YENU NA
KUKUTIMIZIENI NEEMA YANGU NA NIMEKUPENDELEENI
UISLAMU UWE DINI YENU ………….” (5:3)
elewa na ufahamu kwamba kuishi nje ya dini hii
ni kulikana umbile lako kwani UISLAMU NI HAKI
YAKO YA KUZALIWA uliyopewa hadiya (zawadi) na
Mola Muumba wako.
|