Wapatao
(wenye kurithi) robo (1/4) na sharti za kurithi kwao hiyo robo:
Katika
mbea za warithi, wanao stahiki kupata robo (1/4) ya tarika, ni watu
wawili:
MUME:
Mume
wa maiti anastahiki kurithi robo ya mali yote iliyo achwa na marehemu
mke wake, kwa sharti ya kuwa marehemu asiwe ameacha:
Mtoto
wake mwenyewe, au
Mtoto
wa mtoto wake mwanamume na kwenda chini kwa kupitia wanamume watupu.
Ni
mamoja mtoto aliye achwa na marehemu, ni wa mume huyu (mrithi) au si
wake, na ni sawa sawa mtoto huyo ni wa kike au wa kiume.
Na
dalili/ushahidi wa hili, ni kauli yake Allah Atukukiaye: “...WAKIWA
NA MTOTO BASI FUNGU LENU NI ROBO YA WALICHO KIACHA...”. [04:12]
Tumesha
tangulia kusema na tunasema tena hapa: Ya kwamba mtoto wa mtoto wa
kiume (mjukuu wa maiti kwa mtoto wake wa kiume), ni kama/sawa na
mtoto wake maiti. Usawa huo ni katika kurithi, hajbu (kuzuia kurithi)
na katika uasaba.
MKE/WAKE:
Mke/wake
wa marehemu anastahiki/wanastahiki kupata robo ya tarika, kwa sharti
kwamba marehemu hakuacha:
Mtoto
wake mwenyewe, au
Mtoto
wa mtoto wake mwanamume, na kwenda chini kwa kupitia wanamume
watupu. Japo huyo mtoto/mtoto wa mtoto wake huyo hakuzaa na mke/wake
hao.
Na
ushahidi wa hili, ni kauli yake Allah Atukukiaye: “...NA WAKE ZENU
WATAPATA ROBO MLICHO KIACHA, IKIWA HAMNA MTOTO...”. [04:12]
Wapatao
thumni (1/8) na sharti za kurithi kwao hiyo thumni:
Anaye
rithi thumni katika tarika ya maiti, ni mke/wake. Fungu la wake ni
hiyo hiyo thumni hata kama watakuwa ni wane, watagawana hiyo.
Mke/wake watarithi thumni kwa sharti ya kwamba maiti ameacha:
Mtoto
wake mwenyewe, au
Mtoto
wa mtoto wake mwanamume, na kwenda chini kwa kupitia wanamume
watupu.
Ni
mamoja huyo mtoto au mtoto wa mtoto mwanamume wa marehemu, ni
mwanamume au mwanamke.
Dalili
ya hili, ni kauli yake Allah Ataadhamiaye: “MKIWA MNA MTOTO BASI
SEHEMU YAO NI THUMNI YA MLICHO KIACHA...”. [04:12]
SOMO
LA SABA
Wapatao
theluthi mbili (2/3) na sharti za kurithi kwao hizo theluthi mbili:
Wanao
rithi theluthi mbili katika warithi, ni mbea nne za wanawake, na kila
mbea inazo sharti zake stahikishi, tunazitaja kama ifuatavyo:
BINTI
WAWILI NA ZAIDI WA MAITI:
Kumeshurutizwa
katika kurithi kwao theluthi mbili ya tarika, sharti moja tu, nalo ni
kutokuwepo na ndugu yao mwanamume (Asaba) – ambaye ni mtoto
mwanamume wa maiti.
Na
ushahidi wa kurithi kwao hizo theluthi mbili, ni kauli yake Allah
Atukukiaye: “...NA IKIWA WANAWAKE ZAIDI YA WAWILI, BASI WATAPATA
THELUTHI MBILI ZA ALIZO KIACHA MAITI...”. [04:11]
“Na
Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-aliwahukumia mabinti wawili
wa Sa’ad kupata theluthi mbili ya tarika ya baba yao”. Tirmidhiy
[2093] & Al-Haakim [04/334]-Allah awarehemu.
BINTI
WAWILI WA MTOTO MWANAMUME WA MAITI, NA KWENDA CHINI KWA KUPITIA KWA
WANAMUME WATUPU:
Hawa
watastahiki kurithi theluthi mbili kwa kupatikana sharti mbili hizi:
Maiti
asiwe na mtoto wake mwenyewe, au mtoto aliye karibu kwa daraja
kuliko yeye.
Wasiwe
pamoja na ndugu mwanamume, wa daraja moja (ambaye ni Asaba).
Na
dalili ya mabinti wa mtoto mwanamume wa maiti kurithi theluthi mbili,
hakika si vinginevyo ni qiyaasi kilicho twaliwa kwa mabinti wa maiti
mwenyewe (shangazi zao hao watoto). Au dalili ni kule kuingia kwao
chini ya tamko “MABINTI”, kwa kujengea hoja ya kwamba tamko hilo
hutumika katika hakika yake na katika majaazi (uazimwa) yake.
DADA
WAWILI NA ZAIDI WA MAITI WA KWA BABA NA MAMA (SHAQIQA):
Hawa
wanarithi theluthi mbili kwa sharti tatu:
Wasiwe
pamoja na ndugu mwanamume (kaka), wa daraja moja (ambaye kwao ni
Asaba).
Maiti
asiwe na mtoto wake mwenyewe. Au mtoto wa mtoto wake mwanamume na
kwenda chini kwa kupitia wanamume watupu.
Maiti
asiwe na baba au babu.
Na
dalili ya kurithi kwao theluthi mbili, ni kauli yake Allah
Ataadhamiaye: “...NA IKIWA WAO NI NDUGU WA KIKE WAWILI, BASI
WATAPATA THULUTHI MBILI ZA ALICHO ACHA MAITI...”. [04:176]
DADA
WAWILI NA ZAIDI WA MAITI WA KWA BABA TU:
Hawa
watarithi theluthi mbili kwa sharti nne; zile tatu tulizo tangulia
kuzitaja kwa madada shaqiqa. Na sharti ya nne inayo ongezeka, ni:
Maiti kutokuwa na ndugu mwanamume wa kwa baba na mama au ndugu
mwanamke wa kwa baba na mama.
Na
dalili ya kurithi dada wawili wa maiti wa kwa baba tu, ni Ijmaa.
Kwani Ijmaa imekongamana ya kwamba aya hiyo iliyo tangulia kutajwa
hapo juu, hakika si vinginevyo, imeshuka ikiwakhusu dada wa kwa baba
na mama (SHAQIQA) na dada wa kwa baba tu, bila ya dada wa kwa mama.
Imepokewa
kutoka kwa Jaabir bin Abdillah-Allah amuwiye radhi-amesema: Niliugua,
akaja Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-kunikagua (kunijulia
hali), akanikuta nimezimia. Akaja akiambatana na Abubakar na Umar
wakitembea kwa miguu. Basi Mtume wa Allah-Rehema na Amani
zimshukie-akatawadha, kisha akanimwagia maji yake ya udhu,
nikazinduka. Nikasema: Ewe Mtume wa Allah! Nihukumu (nigawe) vipi
mali yangu? Au nifanyeje katika mali yangu? Mtume hakunijibu kitu. –
Na alikuwa na dada tisa – Mpaka ilipo teremka aya ya mirathi:
{WANAKUOMBA UHUKUMU; SEMA: ALLAH ANAKUPENI HUKUMU JUU YA MKIWA...”.
[04:176]
Tirmidhiy
[2098]-Allah amrehemu.
Ukamilifu
wa aya: “...IKIWA MTU AMEKUFA, NAYE HANA MTOTO, LAKINI ANAYE NDUGU
WA KIKE, BASI HUYO ATAPATA NUSU ALICHO ACHA MAITI. NA MWANAMUME
ATAMRITHI NDUGU WA KIKE IKIWA HANA MWANA. NA IKIWA WAO NI NDUGU WA
KIKE WAWILI, BASI WATAPATA THULUTHI MBILI ZA ALICHO ACHA MAITI. NA
WAKIWA NDUGU WANAUME NA WANAWAKE, BASI MWANAMUME ATAPATA SEHEMU ILIYO
SAWA NA YA WANAWAKE WAWILI. ALLAH ANAKUBAINISHIENI ILI MSIPOTEE; NA
ALLAH NI MJUZI WA KILA KITU”.
Jaabir-Allah
amuwiye radhi-amesema: Aya
hii imeshuka ikinikhusu (kwa sababu yangu).
Wapatao
theluthi moja (1/3) na sharti za kurithi kwao hiyo theluthi:
Wanao
pata fungu la theluthi moja (1/3) miongoni mwa warithi, ni wawili tu,
nao ni:
MAMA:
Mama
wa maiti, atarithi theluthi ya tarika ya mwanawe kwa sharti mbili
hizi:
Maiti
asiwe na mtoto wake mwenyewe. Au mtoto wa mtoto wake mwanamume, na
kwenda chini kwa kupitia wanamume watupu.
Maiti
asiwe na ndugu mwanamume au mwanamke zaidi ya mmoja. Wakiwa ndugu
hao ni wa kwa baba na mama (MASHAQIQI), au wa kwa baba tu, au wa kwa
mama tu.
Dalili
ya mama kurithi theluthi moja kwa sharti hizi tulizo zitaja, ni kauli
yake Allah Ataadhamiaye: “...AKIWA HANA MTOTO, NA WAZAZI WAKE
WAWILI WAMEKUWA NDIO WARITHI WAKE, BASI MAMA YAKE ATAPATA THULUTHI
MOJA...”. [04:11]
NDUGU
ZAIDI YA MMOJA WA KWA MAMA TU; WANAMUME AU WANAWAKE:
Ndugu
wa maiti wa kwa mama yake wanarithi theluthi ya tarika ya marehemu
ndugu yao. Wote hawa wanamume na wanawake watashirikiana kurithi hiyo
theluthi (1/3) kwa usawa; bila ya tofauti baina ya wanamume na
wanawake. Watapata theluthi kwa sharti zifuatazo:
Maiti
asiwe na mtoto wake mwenyewe. Au mtoto wa mtoto wake mwanamume na
kwenda chini kwa kupitia wanamume watupu.
Maiti
asiwe na baba au babu.
Dalili
ya kurithi kwao theluthi, ni kauli yake Allah Ataadhamiaye: “...NA
WAKIWA ZAIDI KULIKO HIVYO, BASI WATASHIRIKIANA KATIKA THULUTHI”.
[04:12]
Na
ushirikiano huu unao tajwa na aya, unahukumia usawa baina yao, kama
tulivyo kwisha kusema.
Naam,
hivyo ndivyo ilivyo, lakini babu naye anarithi theluthi katika baadhi
ya hali zake anapo kuwa pamoja na ndugu. Ufafanuzi wa hili utaelezwa
katika mlango wa babu na ndugu, INSHALLAH.
|