|
1.
a)Mwenyezi
mungu amewaumba majini na watu ili wamwabudu. Na
katika hao majini wapo wanaomcha Mungu na
wanaofanya kinyume na hayo.Sasa majini haohao
huwa wanaishi na binaadam katika hali ya kawaida
na huweza kuwazuilia hao wanadam kupata mahitaji
yao kama vile kufanya kazi za kidunia na
mambo mengine mengi. Je! mtu ambaye amepatwa na
hali kama hii akienda kwa wataalam ambao
wanaweza kuwasaidia nini hukum yake?
Na Mtume Muhammad amesema atakayekwenda kwa
mganga wa kienyeji na akayasadiki yale anayosema
mtu huyo, basi amekfueu aliyoteremshiwa yeye
yaani Qur'an tukufu, Je! nini utaratibu wa hali
hii
2.
suali
langu nikuwa hukmu ya yazid bin muawiya ni
gani?twaambiwa alikuwa mlevi,alimuuwa Husain,na
hakuwa muadilifu.ni vipi masala haya?
3.
Mimi
niko nje ya Nchi yangu, pia nafanya kazi katika
Duka, na kazi yangu ni msafishaji Au (CLEANER)katika
duka hilo kunauzwa ulevi,na nyama za nguruwe.
Wakati wowote ule huwa huwajibika kusafisha
panapovunjika chupa ya ulevi, au kuondosha
mifuko ya takataka za Busha ambapo panauzwa hio
nyama ya nguruwe na hunibidi kutamata na
kusafisha mara kwa mara.Pia choo havina maji
hutumia karatasi
tu.
Pia hakuna mahala hata pakuweza kusali kwa
wakati wote unapokuwa kazini.
SUALA
1.Sala zangu zote huzisali baada ya saa za kazi
jee inafaa kusali hivyo?
2.Kwasababu baadhi ya wakati huwezekana kukamata
mifuko ndani yake mulikuwa na nyama ya nguruwe,
jee nikijitoharisha inatosha na kusali?
Naomba unifafanulie masuala yangu kwa ufasaha
zaidi
- Na
katika jumla ya riwaya zilizopokelewa kwamba
Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie
amesema : “ Ye yote mwenye kumuamini Allah
na siku ya mwisho basi asivae hariri
wala dhahabu.” Al-musnad {Musnadul–Imam
Ahmad} sas hapa ni yeyote ama mwanaume
tu naomba mnieleweshe
- Ukijua
kwamba mwanaume anazungumza na
mwanamke kwenye "email. Na huyu
mwanamke siomslamu. Je nifanye nini.
Kwasababu na
jua ataenda na wataonana. Ni fanye
nini?
- JE?
SWAHABA NI NANI ILI AITWE SWAHABA, AWE NA
SIFA GANI?
- suala
langu ni hapa Oman mtu akifa akisha kukoshwa
huvalishwa sanda kisha anavalishwa nguo zake
kiasi mbili au tatu na nyengine anazikwa
nazo,wanasema ni lazma hivo jee kweli
inajuzu?
suala la pili pia wanasema kutahiriwa mtoto
mwanamke ni lazma na imetajwa kwenye kurani
jee ni kweli?
- MUISLAMU
INAMJUZIA KUTIA JINO LA KUBANDIKA IKIWA SI
LA DHAHABU.
- je
inafaa kusali na nguo ambayo umepaka perfume
ambayo ni ya spray na sio mafuta mazito kama
haludi
- mimi niliaapa kuwa sitafanya jambo fulani lakini nimelifanya je natakiwa
nifanye nini wakati nimeapa kwa mola wangu
JIBU
Endelea
Mbele
|