Makala
Mwanzo
Uislamu-Utangulizi
Fiqhi na Sheria 
Akhlaaq-Tabia
Sira ya Mtume
Nasaha za dini
Maswali na Majibu
Uliza Suala la dini
Jiunge na Mtandao

 

  MASWALI NA MAJIBU-Ndoa na Talaka  


Ndoa na Talaka -Sehemu ya Sita                              
  1. Habari za kazi pole na majukumu mimi nina swali
    kidogo,nauliza mvulana amemchumbia msichana ili amuoe
    bahati mbaya baada ya kukubaliwa posa yake wakazini
    mvulana na huyo msichana na akapata mimba sasa yule
    mvulana kuona hali imekuwa hivyo akaamua kwenda kwao
    ili aoe mambo yaishe, sasa ndoa yao inakubaliwa na
    Mwenyezi Mungu ama la naomba ufafanuzi mzuri inshallah
    ni hilo tu sina la zaidi ahsante.

  2. Mimi ni mwanamke, Nina haki ya kudai talaka iwapo sitendewi haki na mume wangu? Kama ninayo, nitumie hatua zipi? Kama Sina Nifanye nini? 

  3. swali langu ni hili pindi mwanamke akiacha sala imeamriwa kuwa aambiwe mara tatu na mumewe kama hakusikia ahamwe kitandani na ni hukumu gani juu ya mwanamume? pia huwenda nikawa  nimekosea kufafanua swali naomba mnisaidie

  4. 1.nataka kujua ushahidi wa mwanaume kuzini.ili ushahidi huo umtie hatiani.
    2.je katika hukumu ya kiislamu kukata rufaa kunakujaje?ikiwa hukumu ya kwanza tayari ni hakika katika sharia kiislamu

  5. kuwa akiwa mumeo haswali analewa jee - kwa sisi wanawake tufanye nini kukaa nae mume huyu ni halali or haramu ? kama ni haramu pia kudai talaka nimesikia kuwa unaingia motoni moja kwa moja. kwani talaka ni halali lakini Allah anaichukia. sasa naomba nasiha. na mimi katika wanawake wanoimani kwani sasa ni mwaka wa 18 hali ndio hii. nasubir naamin faraja iko karibu lakin ni taaban lakin bado nasubiri kama kuna dua naomba mnisaidie ndugu zangu. nakungoja jawabu yenu.

  6. Napenda kuuliza masuala ya haki za ndoa.
    (a) Inapasa mume na mke kuishi mbalimbali kwa muda wa zaidi ya miaka miwili bila ya sababu yoyote?
    (b) Mume anaeitelekeza familia yake bila ya kutoa matumizi ya chakula na malazi kwa muda wa mwaka mmoja,jee,mwanamke atahisabiwa kama bado ni mke au kaachika?
    (c) Mwanamume asiekua na nguvu za kiume inampasa kuoa?

  7. naomba kuuliza suala langu hili, kuhusu kujitia manukato, mume amehawil sana kuzungumza na mkewe kuhusu akitoka nje asijitie mkewe manukato ya aina yoyote udi au mafuta, na mwanamke jawabu hawezi kutoka bila kujitia manukato na mume amechoka kumkataza, sasa analo ogopea asije akavunja ndoa juu yao, tunaomba suluhisho la watu hawa wawili baina ya mume na mke. ni nini? 

  8. ikwa mtu anamtiii mumewe na mumewe anakuwa anamdhania maovu , kama anazini akirudi nyumbani kutazama nyumba nzima kama mkewe kaeka mtu , au akirudi nyumbani anamcheki nyweli kama zimekoshwa , hee hebu nisaidieni mtu kama huyo mwanamke afanye nini na anakuwa taabani na mambo anayofanya mumewe

  9. Nimeolewa na mume ambaye alisilimu miaka 12 iliyopita,kabla hajanioa.
    Aliachana na mkewe wa Kikristo kabla hajawa Muislam,ambaye wakati anamuoa alimkuta na watoto 2 wa Kikristo na aliishi naye kwa miaka 3 tu na kuachana.Sasa,baada ya miaka 12,ameanza kuwasiliana tena na wale watoto wake wa kufikia,Kiasi cha kuwapeleka cinema wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.Mimi niliona siyo sawa Kiislamu,na tulienda kwa Imamu,lakini Imamu kasema si Haramu yeye kujihusisha na wale watoto.
    Je,hii ni kweli? mbona tumeelezwa kwenye sura ya Al I'mran aya ya 100,kuwa tusijihusishe nao na sura nyinginezo pia?
  10. Baada ya kufanya ndoa na mwanamke asiye mwislamu, kubahatika kupata watoto na mwishowe kufikia mfarakano kuachana kisheria kwa nchi tuishiyo. Na kwamba yote  tangu wakati ndoa hata kuachana kwetu kumefanyika nje ya dini yaani hakuna sheikh wala kadhi aliyehusika, bali kufanyika kama vile katika ofisi. Je inanibidi nifanye nini kuhusu watoto baada ya kuachana na mama mtu?


 

JIBU

 

Rudi Nyuma                                                  


| Tuandikie |