Makala
Mwanzo
Uislamu-Utangulizi
Fiqhi na Sheria 
Akhlaaq-Tabia
Sira ya Mtume
Nasaha za dini
Maswali na Majibu
Uliza Suala la dini
Jiunge na Mtandao

 

  MASWALI NA MAJIBU-Zaka  


Zaka-Sehemu ya Kwanza                              
 
  1. Shekh Nakuomba Saana msaada wako kwa kutufafanulia aya hizi zifuatazo nazo
    ni: Qurani 9:60, 9:103, na 2:280. katika eneo hili la hapa keko ninaposali kumetokea kutoelewa baada ya  kuchanganywa na madai ya kwamba:

    1. ZAKA na SADAKA ni kitu kimoja -katika jinsi-ya-kutolewa na watumiaji-pia.

    2. Na kwamba ikiwa mtu akikusudia kukupa/kukuzawadia hata chungwa-moja-tu na  akatamka neno 'SADAKA' basi inakuwa ni kharamu kula ikiwa wewe sio miongoni mwa Fakiri au Masikini n.k kwa mujibu wa Qrn 9:60. Eti kwa ufafanuzi unavyodai.
    ** Na hali hii ilianzia wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani kidogo kidogo
    wakati huo kulikuwa na muislamu aliyeamua kugawa futali kwa baadhi ya
    misikiti na wetu ukawa ni mmoja wapo, Sasa ikawa imamu wetu anapotangazia
    kuwa "Jamanie kuna SADAKA ya futali katika msikiti wetu kwahiyo waislamu
    tuhudhurieni katika kupata chochote kilicho andaliwa na muislamu mwenzetu
    Inshaallah."
    Basi mzozo ulianza polepole kwamba ukitamka neno SADAKA 'kama atakula
    muislamu ambaye anaouwezo wa kupata futali basi ni KHARAMU-KULA maadamu limetamkwa tu neno SADAKA. Yafaa itamkwe IK-RAM!!!. Au ukitaka kumpa  muislamu mwenzio kitu, Basi useme hivi: "Aisee nakukirimu kitu kadha.." Na wala usiseme nakupa SADAKA yangu kitu Kadha..!!!

    2. Na maneno haya SADAKA na ZAKA yanafafanuliwa kama ifutavyo:
    *Sadaka na Zaka nikitu kimoja tu wala havina utofauti wowote -hata katika
    kutolewa kwake.
    *Sadaka ni kusema ukweli, na Zaka ni Kutakasika. kwa mujibu wa Qrn. Kwahiyo
    mtu anapotangaza mali yake ki-ukweli kabisa hiyo huitwa SADAKA, na mtu
    anapolipa zaka ya halali ndiyo kutakasika!!!.
    Kwahiyo imedaiwa kwamba Zaka na Sadaka ni kitu kimoja tu na wapewaji ni kwa mujibu wa Aya hizo hapo juu hasa Qrn 9:60.

    <>Na ama baadhi yetu tumeamua kulifuatilia swala hili lakini tunagonga ukuta
    kutokana na udhaifu wa vitabu na hasa elimu ndogo ya uchambuzi qurani kwa
    kina.
    --------------------------
    KWAHIYO SHEKH: NDIYO MAANA MIMI PAPOJA NA WAISLAMU WENZANGU TUMEAMUA
    TUKUULIZIE WEWE NA UTUSAIDIE JUU YA MZOZO HUU KUPITIA MASWALI YETU HAPO
    CHINI:

    1 Nini Maana, Na matumizi ya maneno haya: SADAKA na ZAKA?
    2 ZAKA inatolewaje? na sadaka?
    3 Je, Shekh mimi nikiamua kukupa wewe tunda kama mf. wa embe kisha nikatamka kwamba: "karibu sadaka ya tunda". itakuwa wewe kuchuwa ni kharamu maadamu unao uwezo wa kulinunua?
    -----
    4. Mwisho kabisa Nakuomba unisaidie, Website ambayo inayochambua KILA AYA kwa HADITHI, ASS'BABU N-NUZL, MAF-HUMU YAKE, mfano kama tafsiri ya IBUN KATHIIR. Na mengineyo kama Hayo.
    Ikiwa ya Lugha ya i.Kiswahili, ii.Kiingereza, au ii.Kiarabu.

    tumejaribu kuitembele website ya www.al-islam.com: katika hadithi, qurani
    nk. na pia www.islamzine.com lakini hatukupata msaada wowote. Juu ya mada
    hii.

    Tunatarajia jibu lolote kutoka kwako (Hata kwa ufupi tu), ilituweze
    kujikwamua na mashaka haya Inshaallah. Na Hasa tusaidie sana Maombi yetu ya
    nambri 4. hapo juu.

  2. 1. jee zakaa ni halali kutoa kwa asikua muislamu?
    2. vile vile fungu lipi ni kubwa zaidi kwa unapotoa zakaa baina ya muislamu na asiekua muislamu?

  3. Ukiwa unafanya kazi na unapokea mshahara mfano laki moja kwa mwezi je kuna haja za kuzitolea zaka.

  4. Swali langu linahusu Zakaa, Je! Nalazimika kuzitolea Zakaa kwa pesa nnazozidai? na sijui ntalipwa lini?

  5. INAJUZU KUZIGAWA PESA ZA ZAKA YA DHAHABU KATIKA SEHEMU YA NYUMBA 5,LAKINI UKANUNUWA CHAKULA KAWAPELEKEA KATIKA KILA NYUMBA,  ILI KIWAFAE KWENYE HUU MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.  AU LAZIMA ZITOLEWE PESA.

  6. INAWEZEKANA IKIWA KATIKA KILA  MWEZI WA RAMADHANI HUWA NIKITOWA ZAKAA YA DHAHABU.  
    KATIKA MWAKA HUU TUMEPATA MSIBA WA NDUGUYETU AMEWACHA WATOTO WA MAYATIMA WADOGO  HAWAJABALEKH.WATOTO   WA YATIMA WANAISHI KATIKA NCHI YA EST AFRICA.  INAFAA KUTOWA PESA KUWANUNULIA NGUO NA KUWAPELEKEA NGUO ZIWAFAE KWA SKUKUU. INAJUZU BADALA YA KUTOWA HIZI PESA KUWAPA WATU HAPA NCHI ZA GULF,
    TAFADHALI NISAIDIYENI HILI SUALA LANGU.

  7. naomba kuuliza suala langu ni kuhusu almasi, almasi inatolewa zaka.na ikiwa inatolewa zaka inaaanza kutolewa kwa kiwango gani?

  8. Swali langu ni kuhusu Zakaa. Je nina lazima kutoa Zakaa kwa pesa nilizokwishazitolea mwaka uliopita?.
    Kwa mfano Mwaka ulipita nilikua na Shs 10,000/ nikazitolea Zakaa, Na mwaka huu zile pesa zimeongezeka kua Shs 15,000/ Swali ni kua itabidi nizitolee zile zilizoongezeka tu yaani Shs 5,000/ au Zote kwa jumla? Naomba jibu.

  9. Ninauliza ikiwa mimi ni mwanafunzi na nilikuwa nikitenga pesa kadha ninazopewa shule. Je ninao ulazima wa kuzitolea ZAKKA? kwa nini?

  10. Mtoto mchanga aliyezaliwa mwezi wa Ramadhani inafaa kumtolea Zakaat Al Fitr?.

 

JIBU

 

                                                                          


| Tuandikie |