Makala
Uislamu-Utangulizi
Fiqhi na Sheria 
Akhlaaq-Tabia
Sira ya Mtume
Nasaha za dini
Maswali na Majibu
Uliza Suala la dini
Jiunge na Mtandao !!!

 

SIRA YA MTUME (SAW)  

"BILA SHAKA MNAO MFANO MWEMA KWA MTUME WA MWENYEZI MUNGU…"Al-qur-an (33:21)

WARUMI WALIUFUATILIA KWA KARIBU MNO MWENDO WA DA'WAH 

 Faida

 

iii.            Warumi waliufuatilia kwa karibu mno mwenendo wa da’awah:

         Kutokana na maelezo yaliyo tangulia itakubainikia kwamba Dola ya Kirumi iliufahamu mlingano (da’awah) wa Uislamu. Na ilikuwa ikiuona kama khatari kubwa iliyo milangoni mwao na ilitambua kwamba mlingano huu utayagusa maslahi yake kwa kiasi kikubwa. Na kwa ajili hii basi, inatakiwa isijisahau au kujilaza. Na pengine vita vya Mu’utah ilikuwa ndio hatua ya kwanza iliyo fanywa na Warumi katika kuiondoshea dola yao khatari hii. Na kwa ajili ya kuuzima mlingano huu ambao waliudhania kuwa ni cheche za moto ambazo kuzimika kwake hakuna muda. Walipo waona waunga mkono wake hawako katika unyonge kama walivyo sawirisha, wakaanza kuiangalia da’awah kwa mtazamo makini. Wakaanza kutafuta khabari zake na kufuatilia nyendo zake kwa makini na karibu. Na walikuwa na majasusi wanao waletea khabari juu ya harakati za da’awah, wakiwaelezea kila kinacho jiri baina ya Mtume wa Allah na maswahaba wake.

Huyu hapa Ka’ab Ibn Maalik-Allah amuwiye radhi-anasimulia kisa chake pale alipo kuwa hakwenda katika vita vya Tabuuk pamoja na Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie. Na Mtume akawakataza watu kuzungumza nae, anasema: Kwamba mfalme wa kabila la Ghassaani alimtumia barua akimwambia: “Ama baad, hakika imetufikia khabari kwamba mtu wako (Mtume) amekukata pande. Na wala Allah hakukuweka katika nchi ya unyonge wala dhiki, basi njoo kwetu tutakuliwaza”. Na ikumbukwe kwamba wakati huo dola ya Ghasaani ilikuwa ni mshirika wa dola ya Kirumi. Lau si kuwa  Warumi walikuwa wakifuatilia khabari za Mtume na maswahaba wake, basi isingelikuwa lazima khabari hii ya Ka’ab kuwafikia. Na wala si kawaida hata kama ingewafikia kwa sadfa, mfalme wa Ghassaani kuishughulikia kwa kiasi hiki.

 

iv.            Msikiti wa Dhwiraari:

         Na katika kisa cha msikiti Dhwiraari, kuna sehemu/upande mwingine unao ashiria uhusiano ulio kuwepo baina ya Warumi na wanafiki miongoni mwa wenyeji wa Madinah. Riwaya zimetaja kwamba Padri Abu Aamir hakuweza kubakia Madinah, baada ya dini ya Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-kudhihiri humo. Akaenda kwa Qayswari mfalme wa Urumi kumuomba msaada dhidi ya Mtume huyu, mfalme akampa ahadi ya kumsaidia na akampa hifadhi kwake. Abu Aamir akaliandikia barua kundi la kaumu yake katika watu wanafiki akiwaahidi kwamba yeye atakuja na jeshi kukabiliana na Muhammad. Na atawashinda na kuizuia itikadi yake hiyo ya Mungu mmoja. Na akawaamuru kumtengenezea ngome atakayo fikia mjumbe wake anaye uleta waraka wake kwao. Na ngome hiyo itakuwa malindizo (mavizio) yake na wao atakapo kuja kwao baadae, ndipo walipo anza kujenga msikiti jirani na msikiti wa Qubaa mpaka wakakamilisha ujenzi wake. Halafu wakamuendea Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-nae akijiandaa kuelekea Tabuuk, wakamwambia: “Ewe Mtume wa Allah! Hakika sisi tumejenga msikiti kwa ajili ya wagonjwa na wenye haja na usiku wa mvua, nasi tunapenda wewe utuswalishe humo (utufungulie msikiti wetu)”. – wakikusudia kwa kitendo hicho, Mtume awakubalie ujenzi wao huo na kuuthibitsha msikiti wao. Mtume wa Allah akawaambia: “Hakika sisi tumo safarini na katika hali ya mshughuliko, tutakapo rudi tutakujilieni na kuwaswalisha humo, Inshallah”.

Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alipo anza msafara kurejea kutoka Tabuuk na haukubakia umbali baina yake na Madinah ila mwendo wa siku moja tu, ukamshukia wahyi juu ya msikiti wa Dhwiraari. Ukielezea juu ya dhamira mbaya ya wajenzi wake katika kuwakufurisha na kuwafarakanisha waumini na mavizio kwa walio mpiga vita Allah na Mtume wake hapo kabla. Mtume wa Allah-Rehema na amani zimshukie-akawatuma watu kuubomoa msikiti huo kabla ya kuwasili kwake Madinah. Na kuhusiana na tukio hili, Allah Taala anasema: “NA WAPO WALIO JENGA MSIKITI KWA AJILI YA MADHARA NA UKAFIRI NA KUWAFARIKISHA WAUMINI, NA PA KUVIZIA KWA WALIO MPIGA VITA ALLAH NA MTUME WAKE HAPO KABLA. NA BILA YA SHAKA WATAAPA KWAMBA: HATUKUKUSUDIA ILA WEMA TU. NA ALLAH ANASHUHUDIA KUWA WAO NI WAONGO. USISIMAME KWENYE MSIKITI HUO KABISA. MSIKITI ULIO JENGWA JUU YA MSINGI YA UCHAMNGU TANGU SIKU YA MWANZO UNASTAHIKI ZAIDI WEWE USIMAME NDANI YAKE. HUMO WAMO WATU WANAO PENDA KUJITAKASA NA ALLAH ANAWAPENDA WANAO JITAKASA”. [9:107-108]

 



 | Tuandikie |