|
I.
Msimamo wa Qur-ani
Tukufu ulikuwa ni mkali mno kwa wale walio acha kwenda katika medani ya vita
bila ya kuwa na udhuru halali:
Kwa ajili hiyo basi, Qur-ani Tukufu ilishikilia
msimamo mkali kabisa kwa wale ambao waliacha kwenda vitani bila ya kuwa na
udhuru – zingatiwa. Ikawalaumu na kuwaumbua, ikawafedhehesha na kuwasifia
uduni, upomoshi wa hima na upuuzi. Na kwamba wao hawayachangamkii ila
manufaa/maslahi ya dunia na malengo yenye kuondoka. Ama amali tukufu na
mambo adhimu, wao si wadau wala watafutaji wake: “NA LAU INGELIKUWA IPO
FAIDA YA PAPO KWA PAPO, NA SAFARI YENYEWE NI FUPI, WANGELI KUFUATA. LAKINI
WAMEONA NI MBALI NA KUNA MASHAKA. NAO WATAAPA KWA ALLAH: TUNGELI WEZA BILA
YA SHAKA TUNGELI TOKA PAMOJA NANYI. WANAZIANGAMIZA NAFSI ZAO. NA ALLAH
ANAJUA KUWA HAKIKA HAO NI WAONGO......NA MONGONI MWAO WAPO WANAO KUSENGENYA
KATIKA KUGAWA SADAKA. WANAPO PEWA WAO HURIDHIKA NA WAKITO PEWA HUKASIRIKA”.
[9:42-58]
Qur-ani ikazidi kuwaaibisha kwa uoga, ushindwa na upite na
kwamba wao si miongoni mwa wenye ukwasi wakati wa shida/matatizo. Na wala si
miongoni mwa wenye msaada wakati wa khatari na wanaipenda raha/starehe iliyo
rahisi kuliko sulubu iliyo tukufu. Na wanaifadhilisha salama iliyo
dhalili/duni juu ya khatari iliyo tukufu: “NA WANAAPA KWA ALLAH KWAMBA WAO
NI KATIKA NYINYI, WALA WAO SI KATIKA NYINYI. LAKINI NI WATU WANAO OGOPA. LAU
KAMA WANGELI PATA PA KUKIMBILIA AU MAPANGO AU MAHALA PA KUINGIA, BASI
WANGELI FYATUKA MBIO KUELEKEA HUKO.........NA INAPO TEREMSHWA SURA ISEMAYO:
MUAMININI ALLAH NA PIGANENI JIHADI PAMOJA NA MTUME WAKE, WALE WENYE NGUVU
MIONGONI MWAO HUKUTAKA RUHUSA NA HUSEMA: TUACHE TUWE PAMOJA NA WANAO KAA
NYUMA! WAMERIDHIA KUWA PAMOJA NA WABAKIAO NYUMA, NA NYOYO ZAO ZIKAPIGWA
MUHURI; KWA HIVYO HAWAFAHAMU” [9:56-87]
Qura-ni ikaibainishia jamaa (kikundi cha waislamu safi walio
kuwa pamoja na Mtume wa Allah kwa dhati ya nia) kwamba hao (wabakiao nyuma)
ni fisadi na uchafu katika jamaa. Na kwamba kukaa kwao wasende vitani,
kulikuwa ni bora zaidi kwa jamaa kuliko kutoka kwao. Na kwamba salama ya
jamaa ni kusafishwa safu zao kutokana na watu hao, kwa sababu wao
hawayaamini malengo ya jamaa na wala hawashirikiani nao kihisia. Na kwa
sababu wao katika jamaa ni vitenda – kazi bomozi na si vitenda – kazi
vijenzi: “NA INGELI KUWA KWELI WALITAKA KUTOKA BILA YA SHAKA WANGELI
JIANDALIA MAANDALIO, LAKINI ALLAH KACHUKIA KUTOKA KWAO, NA KWA HIVYO
AKAWAZUIA NA IKASEMWA: KAENI PAMOJA NA WANAO KAA! LAU WANGELI TOKA NANYI
WASINGELI KUZIDISHIENI ILA MACHAFUKO, NA WANGE TANGA TANGA KATI YENU
KUKUTILIENI FITNA. NA MIONGONI MWENU WAPO WANAO WASIKILIZA. NA ALLAH
ANAWAJUA MADHAALIMU. TANGU ZAMANI WALITAKA KUKUTILIENI FITNA, NA
WAKAKUPINDULIA MAMBO JUU CHINI, MPAKA IKAJA HAKI NA IKADHIHIRIKA AMRI YA
ALLAH, NA WAO WAMECHUKIA. NA MIONGONI MWAO WAPO WANAO SEMA: NIRUHUSU WALA
USINITIE KATIKA FITNA. KWA YAKINI WAO HIVYO WAMEKWISHA TUMBUKIA KATIKA
FITNA. NA HAKIKA JAHANNAMU IMEWAZUNGUKA. UKIKUPATA WEMA UNAWACHUKIZA, NA
UKIKUSIBU MSIBA WAO HUSEMA: SISI TULIANGALIA MAMBO YETU VIZURI TANGU KWANZA.
NA HUGEUKA KWENDA ZAO NA WAMEFURAHI........WATAKUAPIENI KWA ALLAH MTAKAPO
RUDI KWAO ILI MUWAACHILIE MBALI. BASI WAACHILIENI MBALI, HAKIKA HAO NI
NAJSI, NA MAKAZI YAO NI JAHANNAMU, KUWA NI MALIPO KWA WALIYO KUWA
WAKIYACHUMA. WANAKUAPIENI ILI MUWE RADHI NAO. BASI HATA MKIWA RADHI NAO
NYIYE, ALLAH HAWI RADHI NA WATU WAPOTOFU” [9:46-96]
Hivi ndivyo ulivyo kuwa msimamo wa Qur-ani kuwaelekea
wanafiki na watafuta manufaa miongoni mwa wabakiao nyuma wakaepukana na safu
za jamaa. Iliwadunisha na kuwatweza kutokana na hali yao na ikawaweka pale
walipo jiweka wao wenyewe; yaani pamoja na walio bakia nyuma miongoni mwa
wanawake, watoto, washindwa (wagonjwa) na wanyonge. Na ikalifichua suala lao
kwa jamaa na kuihadharisha dhidi ya khadaa zao na ikawaamrisha kujitenga
nao. Na zama walipo kuja kwa Mtume wa Allah-Rehema na Amani
zimshukie-wakitaka udhuru, alikupa nyongo kuwalaumu. Na badala yake
akawakubalia dhahiri ya udhuru wao na kuiacha siri (undani) yao kwa Allah.
Ama wale ambao walijitegemeza kwenye ucheleweshi na
wakalazwa na ulegevu kwa sababu ya uvivu na kupondokea ubwete. Na kujitia
vivulini katika wakati wa joto kali, haikuwasukuma kutenda hivyo shaka yo
yote na wala haukuwapelekea kutenda hivyo unafiki wala vitimbi. Hawa, toba
yao ilikubaliwa na Allah na akampa idhini Mtume wake kuwasamehe. Na
akamuamrisha kuwatakabalia baadhi ya mali zao wanazo zitoa kwa ajili ya
Allah, ili kuzitwahirisha nafsi zao. Na kwa ajili ya kutangaza kukubaliwa
kwao katika safu za jamaa na kuituliza khofu yao kwa kuwaombea kwake. Na
azitulize nyoyo zao kwa kuwaswalia na kwa kurejea msamaha na maghfira ya
Allah kwao: “NA WENGINE WALIKIRI DHAMBI ZAO, WAKACHANGANYA VITENDO VYEMA NA
VINGINE VIOVU, ASAA ALLAH AKAPOKEA TOBA ZAO. HAKIKA ALLAH NI MWENYE KUSAMEHE
MWENYE KUREHEMU. CHUKUA SADAKA KATIKA MALI ZAO, UWASAFISHE NA UWATAKASE
KWAZO, NA UWAOMBEE REHEMA. HAKIKA MAOMBI YAKO NI UTULIVU KWAO. NA ALLAH NI
MWENYE KUSIKIA MWENYE KUJUA. JE! HAWAJUI YA KWAMBA ALLAH ANAPOKEA TOBA YA
WAJA WAKE, NA ANAZIKUBALI SADAKA, NA KWAMBA ALLAH NI MWINGI WA KUPOKEA TOBA
NA MWENYE KUREHEMU? NA SEMA: TENDENI VITENDO, NA ALLAH NA MTUME WAKE NA
WAUMINI WATAVIONA VITENDO VYENU. NA MTARUDISHWA KWA MWENYE KUJUA SIRI NA
DHAHIRI; NAYE ATAKUAMBIENI MLIYO KUWA MKIYATENDA: [9:102-105]
II.
Toba ya Ka’ab Ibn
Maalik na wenzake wawili:
Na walikuwemo miongoni mwa walio bakia nyuma
wasende vitani, watu watatu walio mwambia ukweli Mtume wa Allah-Rehema na
Amani zimshukie. Hawa hawakutunga uwongo na wala hawakupindua maneno,
wakaliweka suala lao mikononi mwa Allah awahukumu atakavyo. Watatu hawa ni;
Hilaal Ibn Umayyah, Muraarah Ibn Rabee na Ka’ab Ibn Maalik. Na katika kisa
cha Ka’ab Ibn Maalik – kama kilivyo pokewa na wapokezi wengi – kuna
sura/picha iliyo kwenda kina ya nafsi yenye hisia za mbali, iliyo muumini
katika ukweli wake. Na katika ufumbulizi wake, dhiki yake na uhemevu wake,
na katika uwokovu wake na furaha yake, na katika usafi wa niya yake na toba
yake. Na taswira nyingine ya jamii ya Kiislamu katika kupanda kwa mwamko
wake na utukufu wa kudiriki kwake mambo na hisia zake kali katika kuelewa
dhambi ya mwenye dhambi na toba ya mtubiaji. Ka’ab Ibn Maalik anasema:
“...ilikuwa katika khabari yangu pale nilipo bakia nyuma na Mtume wa
Allah-Rehema na Amani zimshukie-nisende pamoja nae katika vita vya Tabuuk.
Kwamba katu mimi sikuwa mwenye nguvu mno na mwepesi sana, kuliko pale nilipo
bakia nyuma nisende pamoja naye katika vita hivyo. Wallah, sikupata
kukusanya kwangu kabla ya vita hivyo vipando viwili hata nikavikusanya
katika vita vile. Na wala Mtume wa Allah-Rehema na Amani
zimshukie-hakukusudia vita ila alificha muelekeo wake. Mpaka vikawa vita
vile, Mtume wa Allah akapigana katika joto kali na akaikabili safari ya
mbali na maadui wengi. Basi Mtume akawawekea wazi suala lao (ya kuwa
wanaelekea wapi) ili wajiandae vya kutosha na safari hiyo, akawaeleza
muelekeo wake alio ukusudia. Na waislamu walio kuwa pamoja na Mtume wa Allah
ni wengi, basi hapana mtu ye yote aliye taka kughibu (kutoweka) ila
alidhania kwamba hili litafichikana maadam wahyi haujateremka kutoka kwa
Allah aliye tukukia.
Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-akapigana vita vile
wakati wa upendezi wa matunda na vivuli vya miti. Mtume wa Allah na waislamu
walio kuwa pamoja naye wakajiandaa, nami nikadamka kujiandaa pamoja nao,
basi hurudi na ilhali sijakidhi cho chote, basi hapo hujisemea: Mimi ni
muweza juu ya hilo nikitaka. Basi hali hiyo haikuacha kunitambalia mpaka
watu wakamaliza maandalizi yao na kuwa tayari kuondoka. Mtume wa
Allah-Rehema na Amani zimshukie pamoja na waislamu wakaanza kuondoka nami
nikiwa sijakidhi cho chote katika matayarisho yangu. Nikajiambia:
Nitajiandaa baada yake kwa siku moja au mbili, halafu nitawakuta njiani.
Basi baada ya kuondoka, mimi nikadamka kujiandaa, sikukidhi cho chote,
nikadamka tena halafu nikarudi bila ya kufanya cho chote. Basi nikaendelea
hivyo mpaka wakaenda zao haraka na ikanipita fursa ya kuvidiriki vita vile.
Nikakusudia kusafiri ili niwadiriki njiani – eeh laiti mimi ningeli fanya
hivyo – lakini hilo halikukadiriwa kwangu. Basi ikawa ninapo watokea watu
baada ya kuondoka kwa Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie.
Ikanihuzunisha kwamba mimi sioni kwangu kigezo ila mtu atuhumiwaye kwa
unafiki au mtu miongoni mwa walio pewa udhuru katika wanyonge. Na Mtume wa
Allah hakunikumbuka mpaka alipo fika Tabuuk, akauliza ilhali akiwa amekaa na
maswahaba Tabuuk: “Amefanya nini Ka’ab Ibn Maalik?”, akajibu mtu katika
Baniy Salamah: “Ewe Mtume wa Allah! Kumemshughulisha kujiona kukamzuia
kutoka”. Muaadh Ibn Jabal akasema: “Maneno mabaya yaliyoje uliyo yasema!
Wallah, ewe Mtume wa Allah! Hatujui kuhusiana naye ila kheri tupu”. Mtume wa
Allah akanyamza kimya, hakusema lo lote.
Ka’ab anaendelea kusema: “Zama ilipo nifikia khabari kwamba
Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-anarudi kutoka Tabuuk, ukanipata
mtapo tapo wa moyo. Nikaanza kukumbuka uwongo nikijisemea: Ni kipi kitakacho
niokoa na ghadhabu yake kesho? Nikamtaka msaada juu ya hilo kila mwenye
busara katika watu wangu. Palipo semwa kwamba Mtume wa Allah amekaribia
kuingia Madinah, batili yote ikaniondokea na nikatambua kwamba mimi
sitaokoka kwake kwa kusema uwongo, nikatinda kumwambia ukweli. Mtume wa
Allah-Rehema na Amani zimshukie-akafika na ilikuwa ni ada yake anapo toka
safari hufikia msikitini kwanza akaswali rakaa mbili. Kisha ndipo hukaa kwa
ajili ya kuwasikiliza watu, alipo keti wakamjia walio bakia nyuma wasende
vitani, wakitoa udhuru kwake na wakimuapia. Na walikuwa kiasi cha watu
themanini na kitu, Mtume wa Allah akazikubali dhahiri zao na akawafanyia
baia na kuwaombea maghfira. Na akazitegemeza na kuziacha siri zao kwa Allah,
mpaka nikaja mimi mbele yake....
|