|
Kitambo kifupi baada ya Bwana Mtume-Rehema na
Amani zimshukie- na jamaa zake kutoka katika kambi ya Mzee Abuu Twaalibu ambako wali
zuiliwa na kuondoshwa kwa vikwazo dhidi ya yalitokea matukio mawili ambayo yalimuathiri
sana Mtume wa Mwenyezi Mwenyezi Mungu. Matukio haya ya huzuni si mengine bali ni ile tukio
la kufiwa na Ami yake Mzee Abu Twaalib kisha kuandamiwa na kifo cha mkewe Bi Khadijah
baada ya mwezi ya mwezi mmoja Mzee Abuu Twaalib aliposhikwa na maradhi na akafa kuacha
hali ya uadui baina yao na Mtume akiendelea bila ya kupatiwa ufumbuzi muafaka. Mtu pekee
waliyeona kuwa ndiye mwenye mwenye ufumbuzi wa tatizo hili ni Mzee Abuu Twaalib ambaye ni
kiongozi kwa upande wao na upande wa pili ni Ami na mlezi wa Mtume. Kwa hivyo wa kaamua
kumuendea ili afanye suluhu kati yao na mwana wa nduguye. Mwana sira mashuhuri Ibn Ishaq
Allah amrehemu - anaelezea na kusimulia hali ilivyokuwa: (Abuu Twaalib alipozidiwa na
maradhi makurayshi waliteta: Hamza na Umar wamekwishasilimu na suala la (dini ya)Muhammda
limeshaenea na kutangaa katika makabila yote ya makurayshi. Basi tumuendee Mzee Abuu
Twalib atupe dhamana ya mwana wa nduguye". Makurayshi watukufu wakaenda kawa Mzee
Abuu Twaalib na kumwambia "Ewe Abuu Twaalib, hadhi yako kwetu ni kama uijuavyo, na
unaiona hali uliyonayo, inatisha naunajua wazi mzozo uliopo kati yetu na mwana wanduguyo.
Basi sisi tunakuomba umuite, uchukue dhamana kwetu na kwake kwake ili yeye aache kutukera
nasi tuache kumkera, yeye atuache na dini yetu na sisi tumuache nadini yake Abuu Twaalib
baada ya kusikiliza kwa makini shauri waliokuja nalo jamaa zake makurayshi, akamtuam
mjumbe kwenda kumuita Bwana Mtume. Mtume alipofika , Ami yake akamwambia : "Ewe mwana
wa ndugu yangu, hawa watufufu miongoni mwajamaa zako wamekusanyika kwa ajili yako ili
wakupe (ahadi) nawe uwape (ahadi )". Bwana Mtume -Rehema naAmani zimshukie -akasema :
"Ewe Ami yangu neno moja tu mlilopewa, mtawamiliki waarabu kwa neno hilo na wasio
waarabu watakufuateni kwa sababu ya neno hilo". Abu jahliaksema : "naam tuambie
hata maneno kumi !" Mtume akasema Laa Ilaaha illal-laah {Hapana mola apasaye
kuabudiwa kwa haki ila Allah} na mviache mnavyoviabudu kinyume cha Allah. Makurayshi
wakapiga makofi (kwa kustaajabu)na wakasema: "Ewe Muhammad, hivi unataka kuwafanya
miungu wote kuwa Mwenyezi Mungu mmoja tu? Hakika jambo lsko hili ni jambo la ajabu sana!
Kisha wasemezana wao kawa wao: " Hakika wallah !mtu huyu {yaani Mzee Abuu Twalib}
hawezi kukupeni shaurijema la kukuridhishenibasi enendeni zenu na muendelee na kuifuata
dini ya baba zenu mpaka pale Mwenyezi Mungu atakapohukumu baina yenu na yeye
{Muhammad}". Halafu wakatawanyika.
Baada ya hapo Mzee Abuu Twaalib hakuishi muda mrefu akafariki dunia
huku akifuatiwa na Bi khadijah mkewe Mtume.
Baada ya misiba miwili hii iliyompata, Mtume akawa anakabiliana ana kwa
anana maadui zake bila ya kuwa na ngome na mihimili yake hii miwili ; Ami yake na mkewe
hii ndiyo fursa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa sana na makurayshi, fursa ya ushindi
dhidi ya Muhammad asiye na mtu wa kumuhami wala kumtetea. Mzee Abuu Twaalib alikuwa ni
ngome madhubuti iliyomzunguka Mtume pande zake zote na hivyo kumzuilia na kumuondoshea
maudhi na madhara yote. Ama Bi Khadijah alikuwa ni muhimili wake wandani ambapo hapo
alipata utulivu na amani baada ya maudhi na makero ya makurayshi Bibi huyu mwema ndio
lilikuwa kimbilio lake la pekee baada ya dhikina taabu zilompata. Alipokufa Mzee Abuu
Twaalib; Ami yake na Bi Khadijah mkewe, Bwana Mtume akwa amepatwa na misiba miwili mikubwa
ambayo haikumanisha kingine zaidi ya kumpoteza msaidizi{Ami yake} na makimbilio yake
{mkewe}. Ikampata Bwana Mtume huzuni kuu kutokana na misiba hii miwili ambayo iliyofatana
mpaka ukaitwa mwaka ule "mwaka wa huzuni". Naam, kifo cha Mzee Abuu Twaalib
kilikuwa ni msiba mzito kwa Mtume kwani aliikosa ngome imara na madhubuti, kuuondoka kwa
ngome hiyo ni kuwaachia mwanya na upenyo makurayshi kupambana na Mtume kwa urahisi zaidi
kuliko ilivyokuwa wakati wa uhai wa ngome hiyo maudhi na kero na makurayshi kwa Mtume
zikarudifika. Kifo cha Bi Khadijah mkewe pia kilikuwa ni pigo jingine kubwa kwa Mtume,
kifo hiki kiliacha pengo ambalo halikuweza kuzibika katika uhai wote wa Mtume. Ushahidi wa
hilo ni namna ambavyo Bwana Mtume alivyokuwa akimtaja sana kwa wema warehemu mkewe huyu na
kuombea Mwenyezi Mungu mbeleza wakeze wengine mpaka wakawa wanafanya wivu. Naam ni kweli
lazima Mtume awe katika hali hiyo kama binadamu, nabinadamu tu bali binadamu aliyepeaw
jukumu zito na gumu ; jukumu la kufikisha ujumbe wa Mola wake kwa viumbe wake. Kwa nini
isiwe hivyo, uko wapi sasa ule moyo mkubwa wenye dawa ya kumtuliza na kumliwaza baada ya
tabu na ucovu anoupata katika kulitekeleza jukumu alilokabidhiwa na mola wake?!I wapi ile
akili yenye akili sambamba na uoni, akili iliyosimamamemo/makamu ya wazuri mkweli na
muaminifu kwake katika shida na raha?!
Iwapi ile nafsi yenye uonakao na kila aonaye, nafsi iliyobeba
mazitoyake Bwana Mtumena kushirikiana nae katika machungu yake?! Yu wapi Khadijah, yule
mkewe mwema, mtu aliyemwamini pale watu walipomkanusha na kumkataa, mtu aliyemsakisha watu
walipomkabidhisha , mtu aliyemfanya kuwa mkwasi kwa mali yake akaitoa kwake yote kama
alivyotoa nafsi yake?! Li wapi anga lile la liwazo lililokuwa likimfunika kwa mapenzina
huruma na kumpa nguvu mpya za kuweza kukabiliana na viziwiu na kipofu hawa wasio na
akili?! Yote haya yaliyeyuka na kuondoka kwa (na) kifo cha Bi Khadijah na Mzee Abuu
Twaalib, Bwana Mtume akawa sasa hana nje mlinzi, msaidizi na hana ndani mwenye kumliwaza
misba hii miwili ilikuwa ni pigo la ndani na nje. Misiba hii ilibadilikwa muda tabia na
mwenendo mzima wa Bwana Mtume,Mtume akawa ni mtu mwenye tabia ya upweke, anakaa peke yake
muda mrefu na akikaa zaidi ndani bila ya kutoka nje.
Naam ilikuwa ni fursa adhimu kwa makurayshi kupambana na Mtume ana kwa
ana bila ya kizuizi chotechote kweli walizidisha kero na maudhi huku wakiamini kuwa hiyo
ndio njia sahihi itakayowapatia ushindi dhidi ya Mtume. Miongoni mwa maudhi ni kama
inavyosimuliwa na Imam Muslim akipokea kutoka kwa swahaba wa Mtume Ibn Masoud Allah
amridhie- amesema : siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema naAAmani alipokuwa anaswali
katika Al-kaaba Huku Abu Jahli akiwa amekaa na wapambe {wafuasi}wake. Na jana yake
walikuwa wamechinjwa ngamia, Abu Jahli akasema: Nani kati yenu atakaye yaendea matumbo na
uchafu wa ngamia wa baniy fulani, akyechukua akja kumuwekea Muhammad mabegani atakapokuwa
amesujudu? Akainuka mtu muovu mmmoja akaenda akayachukua nakumuwekea Mtume kati ya mabega
yake. Anasema(Ibn Masoud):wakawa wanachekea na kuyumbia huku nakulanami nikiwa nimesimama
ni kiangalia. Lau ningekuwa na nguvu ningeliondosha uchafu ule mgongoni kwa Mtume wa
Mwenyezi Mwenyezi Mungu. Mtume aliendelea kusuju bila ya kunyanyua kichwa chake mpaka pale
msamaria mwema alipokwenda kumpasha khabari hiyo Bi Fatmah binti ya Mtume .Binti huyu
mwema ndiye alikuja na kumuondoshea baba yake uchafu huu, kisha akawagekia mahasimu wake
na kuwashutumu kutokana na kitendo chao hicho kibaya. Mtume alipomaliza kuswali,
aliwaombea dua mbaya wale wote waliofanya kitendo kile kibaya.
Hili ni moja tu miongoni mwa mrorongo mrefu wa matukio ya maudhi na
kero. Wakati mwingine makurayshi walimwagia mtume mchanga kichani, siku moja walimfuata
kwenye Al-kaaba, mmojawao akmrukiana kumkaba shingo nashuka (kishali)yake kwa lengola
kumnyonga mpaka afe. Bahati nzuri aktokea swahibu yake, yule mkwerli Bwana Abuu Bakri
akamsukumia mbali muoniyule, aksema il-hali akilia : "OH! MTAMUUA MTU KWA SABABU TU
ANASEMA MOLA WANGU NI ALLAH?
"[40:28]
Kwa kwelimatendoyao haya ya maudhi na kero yakikuwa na atharikubwa kwa
Mtume,lau si kuwa Mwenyezi Mungu aliuthibitisha moyo wa Mtume wake na kumsaida kwa nguvu
na uwezo wake, maudhi haya yalitosha kabisa kumuyumbisha Mtume na kumfitinisha na dini
yake. Hii ni miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake: "NA HAKIKA WALIKUWA
KARIBU KUKUNGEUSHA NAYALE TULUYOKUFUNULIA ILI UPATE KUTUZULIA BADALA YA HAYA (ya haki
tuliyokuteremshia) NA HAPO BILA SHAKA WANGALIKUKUFANYA RAFIKI (yao mkubwa) NA KAMA
TUSINGALIKUTHIBIBITISHA UNGALIKUWA KARIBU KUWAELEKEA KIDOGO. HAPO BILA SHAKA
TUNGALIKUONJESHA ADHABU KUBWA YAMAISHA (ya hapa ulimwenguni na adhabu kubwa ya maisha
akhera)KISHA USINGEPATA MSAIDIZIWA KUKUNUSURU JUU YETU." [17 73-75]
|