i/
SAFARI YA ISRAA
NA MIIRAJI
Mwaka
wa huzuni ambamo Mtume
aliipoteza mihimili
yake miwili; muhimili wa ndani, mkewe
Bi Khadijah na
Muhimili wa nje Ami
yake Mzee Abuu Twaalib;
Upasito wa watu wa
Makkah na mapokezi mabaya ya watu wa Twaif. Matukio yote
haya yalimtia
Mtume katika hali ya
huzuni kuu, na kumkatisha tamaa na watu wake
kwa kiasi kikubwa sana . Ni
katika hali na mazingira haya ndipo Mwenyezi Mungu
Mtukufu alipomkirimu
Mtume wake safari
ya Israa na Miiraji kabla
ya Hijrah ya Madinah.
Israa ni ile safari ya
Bwana Mtume – Rehema na
Amani zimshukie – kutoka
mji mtukufu wa Makkah usiku mpaka Baaytul-Maqdisi
Jerusalem, Katika
nchi ya Palestine. Ama Miiraji ni ile safari iliyoanzia
hapo katika
Baytil-Muqaddas kuelekea ulimwengu
na anga za juu kabisa
(mbinguni) kuonana na Mola
wake na hatimaye kupewa
zawadi ya
swala tano yeye na
umati wake . Safari ya Israa
imetajwa ndani ya
Qur – ani Tukufu:
UTUKUFU NI WAKE YEYE
AMBAYE ALIMPELEKA MJA WAKE
USIKU (mmoja tu) KUTOKA
MSIKITI MTUKUFU (wa makkah) mpaka MSIKITI WA MBALI (wa Baytul-Muqaddas – Palestine) AMBAO (tumeubariki
na) TUMEVIBARIKI VILIVYOKO PEMBEZONI
MWAKE. (Tulimpeleka Hivyo) ILI TUMUONYESHE
BAADHI YA
ALAMA ZETU.
.HAKIKA YEYE ( Allah)
M MWENYE KUSIKIA ( na ) mwenye
kuona” ( 17:1).
Ama
Safari ya Miraji imepokelewa
katika vitabu sahihi vya hadithi . Hadithi
sahihi zaidi katika
kuitaja safari hii ni ile iliyopokelewa na kuitaja safari hii ni ile
iliyopokelewa na Maimamu
Bukhaariy na Muslim na
Kunakiliwa na Kadhi Iyaadh katika
kitabu chake kiitwacho “Shifaa”. Imepokelewa riwaya kutoka
kwa swahaba wa Mtume : Anasi Ibn Maalik -
Allah amuwiye radhi - amesema
: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu
– Rehema na Amani zimshukie ; aliletwa
buraqu, naye ni mnyama
mkubwa kuliko punda na ni mdogo
chini ya nyumbu. (Spidi yake
anapokimbia) huweka kwato zake ukomo wa macho yake”
Mtume akasema : Nikampanda mpaka
nikafika
Baytul – Muqaddasi , Hapo nikamfunga kwenye kikuku ambacho
walikuwa wakimfungia Mitume (kabla yangu). Kisha nikaingia
msikitini na kuswali humo nakaa mbili halafu nikatoka
ndipo Jibril aliponiletea chombo chenye
pombe na kingine kina
maziwa (nichague)
nikachagua (na kunywa) maziwa. Jibril akasema umechagua jumbile
(umbo). Halafu tukapandishwaa mbinguni, Jibril akabisha hodi akaulizwa U
nani wewe ? Akajibu Jibril, akaulizwa (tena) U pamoja
na nani wewe ? Akajibu Muhammad
. Akaulizwa (tena) : Je ameitwa kuja
huku ? Akajibu , naam ameitwa
. Tukafunguliwa , Kutahamaki huyu ndiye Adam, akanikaribisha na kuniombea
dua njema. Kisha tukapandishwa mpaka uwingu wa pili, Jibril akabisha hodi
akaulizwa : U nani wewe? Akajibu Jibril, akaulizwa (tena) U pamoja
na nani wewe ? Akajibu Muhammad.
Akaulizwa ( tena ) ;Je ameitwa
kuja huku ? akajibu naam
ameitwa. Tukafunguliwa tahamaki niko uso kwa uso na ndugu wawili wa mama
mkubwa na mama mdogo ; Yahyah
na Issa mwana wa Mariam Wakanikaribisha
na kuniombea dua njema. Halafu
Tukapandishwa uwingu wa tatu ( Jibril)
akataja ( maneno ) kama
yale ya mwanzo basi tukafunguliwa
. Kutahamaki huyu ndiye Yusuf naye akiwa
kapewa nusu ya uzuri akanikaribisha na kuniombea dua njema . Kisha
tukapandishwa mpaka
uwingu wa nne , ( Jibril ) akataja ( maneno ) yale yale,
Tahamaki niko ana kwa ana na
Idrisa, akanikaribisha na kuniombea dua njema. Amesema Mwenyezi
Mungu Mtukufu katika Suurati Maryam. “NA
TULIMUINUA DARAJA YA JUU KABISA’
(19:57). Kisha tukapandishwa
mpaka uwingu wa tano akataja maneno yale yale. Tahamaki
niko mbele ya Haruni akanikaribisha na kuniombea dua njema . Halafu
tukapandishwa mpaka uwingu wa sita akataja maneno yale yale
Tahamaki huyu ndiye
Musa akanikaribisha na kuniombea dua
njema. Kisha tukapandishwa mpaka
uwingu wa saba akataja maneno yale
yale. Tahamaki niko ana kwa
ana na Ibrahim akiwa ameegemeza mgogo
wake kwenye (Msikiti wa) Baytul – Maamuri. Msikiti huo huingiwa na
malaika sabini alfu (70,000)
kila siku (wapya wasio
wale waliopata kuingia). Kisha ( Jibril) akanipeleka mpaka penye Mkunazi wa kumalizikia ( mambo yote ) . Majani ya
Mkunazi huo ni kama (Ukubwa wa) masikio ya tembo na matunda yake ni kama
magurudumu. Mkunazi ule
ulipofunikwa kwa amri ya Mola
wangu , Ulibadilika. Basi hakuna yeyote katika viumbe wa Mwenyezi
Mungu anayeweza kuusifia mkunazi huo kutokana na uzuri wake.
Mwenyezi Mungu akanifunulia
hapo aliyonifunulia yaani wahyi na akanifaradhisha mimi na umati wangu
swala khamsini mchana na
usiku. Nikateremka mpaka
kwa Musa akaniuliza Mola wako ameufaradhishia nini umati wako ?
Nikamwambia swala Khamsini akaniambia
rejea kwa Mola ukamuombe akupunguzie kwa sababu umati wako hawataliweza
hilo kwani mimi nimewajaribu Baniy Israil na kuwa na uzoefu nao. Akasema
(Mtume) Nikarudi kwa mola wangu
na kumwambia ewe Mola wangu
Wapunguzie umati wangu, akanipunguzia
Swala Tano (zikabakia arobaini
na tano). Nikarejea kwa
Musa nikamwambia amenipunguzia
tano. Akaniambia umati wako hawataziweza hizo, rudi tena kwa Mola
wake ukamuombe akupunguzie; Akasema
(Mtume) “Nikawa nikienda na
kurudi baina ya Mola wangu Mtukufu na Musa mpaka akasema utakatifu ni
wake; Ewe Muhammad hizo ni swala tano kila mchana na usiku.
Kila swala moja kwa swala kumi basi hizo ni swala khamsini.
Na yeyote atakayekusudia kufanya jambo jema na asilitende,
ataandikiwa jema moja, Na
atakayekusudia kutenda jema na akalitenda ataandikiwa mema kumi,
Na atakayekusudia kutenda na asilitende hataandikiwa chochote.
Na atakayekusudia kufanya ovu na akalifanya ataandikiwa dhambi/baya
moja” Akasema Nikashuka
mpaka kwa Mussa, nikampa khabari ya huko. Akasema rudi tena kwa Mola wako umuombe takhfifu nikamwambia
nimerejea kwa Mola wangu mpaka nimeomuonea haya kisha Bwana Mtume –
rehema na Amani zimshukie akarejea usiku ule ule kulipopambazuka akadamkia
kwenye baraza ya Makurayshi. Abu Jahli Ibn Hishaam akamjia nae
akamuhadithia khabari yote iliyotokea Abu Jahli akaita Enyi Bany Ka’abi
Ibn Luayyi njooni makafiri wa kikurayshi wakamjia, Bwana Mtume anaelezea
khabari ile baada ya kuusikia wakawa wako miongoni mwao waliopiga makofi
na wengine wakawa wameshika vichwa vyao kwa kustaajabu na kupinga. Baadhi
ya watu waliokuwa wamemuamini Mtume waliritadi
na kurudi ukafirini, hawa walikuwa ni wale madhaifu na Imani.
Baadhi ya watu wakamuendea rafiki mkubwa wa Mtume Bwana Abi Bakri
na kumpasha khabari ile. Akamwambia
ikiwa amesema hivyo basi amesema kweli wakamwuliza
Unamsadiki kwa khabari hizi? Akajaribu,
Mimi ninamsadiki kwa khabari za mbali zaidi kuliko hizo (za kwenda
Baytul-Muqaddasi usiku na kurudi hapa usiku huohuo). Tangu siku hiyo ndipo
alipoitwa Abu bakari Sidiyk (Abu Bakri Msadikrishaji). Kisha makafiri wale
wakaanza kumtahini Mtume kwa kumuuliza sifa za msikiti
wa Baytul–muqaddasi na miongoni mwao walikuwepo walioujua.
Ama Bwana mtume alikuwa hapata kuuona kabla ya safari hiyo.
Mwenyezi Mungu akamletea Mtume wake msikiti ukawa mbele ya macho
yake akawa anawasifia mlango baada ya mlango na sehemu baada ya sehemu.
Wakasema ama kwa upande wa sifa tu amepatia kweli.
Sasa tuelezee khabari ya msafara yetu. Walikuwa na misafara yao ya
biashara ikitokea shamu. Bwana
Mtume akawaeleza idadi ya ngamia waliomo katika misafara hiyo na hali yake
na akawaambia itakufikieni siku fulani mchana ikiongozwa na ngamia wa
kijivu. Wakaondola wakiingojea siku hiyo kwa hamu,
akasema mmoja wao siku hiyo wallah Jua hilo limechomoza,
Na mwingine akasema Wallah na msafara huo umeingia na unaongozwa na
ngamia wa kijivu kama alivyosema Muhammad.
Utabiri na ukweli huu wa bwana Mtume haukuwazidishia Mukurayshi ila
kibri na upinzani mpaka wakasema huu ni uchawi wa dhahiri. Asubuhi ya
usiku ule wa safari ua Israaa na Miiraji, Jibril alikuja na akamfundisha
Mtume jinsi ya kuswali na nyakati za swala. Aswali rakaa mbili alfajiri,
rakaa nne adhuhuri na nyingine lasiri na rakaa tatu magharibi na nne
ishaa. Bwana Mtume kabla ya kufaradhiwa suala alikuwa akiswali rakaa
mbili asubuhi na jioni kama alivyokuwa
akiswali Nabii Ibrahimu – Rehema na Amani ziwashukie wote.
|