|
Katika
mwaka uliofuatia kundi la watu wasiopungua kumi na mbili kutoka (Madinah)
lilikuwa ni miongoni ma uma uliohudhuria msimu wa Hijjah kutoka pande
mbalimbali za bara Arabu. Kundi hili lilikusanya watu kumi kutoka katika
kabila la Khazraji na wawili wakiwa ni wa kabila la Ausi. Ausi na Khazraji
ndio makabila makubwa yaliyounda wazalendo wa Yathrib wakati huo. Historia
imetusajili majina ya watu hawa muhimu katika historia nzima ya uislamu,
watu ambao mchango wao umekuwa ni sababu ya kuifikisha uislamu hapa ulipo
leo. Kwa upande wa Khazraji walikuwa ni mabwana:-
-
As’ad
Ibn Zaraarah.
-
Auf
Ibn Al-Haarith
-
Muaadh
Ibn Al-Harith
-
Raajiri
Ibn Maalik
-
Dhakawaan
Ibn Swaamti
-
Ubaadah
Ibn Swaamit
-
Yaziyd
Ibn Tha’alabah
-
Abbaas
Ibn Ubaadah
-
Uqbah
Ibn Aamir, na
-
Qutwabah
Ibn Aamir
ama
kwa upande wa Ausi walikuwa
-
Abul-Haytham
Ibn Tiyhaani
-
Uwaym
Ibn Saa’idah
Kundi
hili lilikutana na Bwana Mtume usiku katika sehemu ijulikanayo kama
“Aqabah”. Hapa ni mahala ambapo shetani hupigwa mawe wakati wa
kutekeleza ibada ya Hijjah tangu zama hizo hadi leo hi. Bwana Mtume katika
mkutano wake huu wa siri na uficho mkubwa na watu hawa kumi na mbili,
aliitumia fursa hii ya pekee kuwapasha zaidi habari za uislamu. Katika
kuhitimisha kwake mkutano huu Mtume aliwataka watu hawa wapeane nae ahadi
ya utii na uaminifu. Nao kutokana na mafundisho ya uislamu yaliyokwishaana
kuziathiri nyoyo zao, bila kusita walikubali. Wakafunga maagano ya utii na
uaminifu kwa mtume wa Allah na maagano haya yakaitwa “Maagano ya kwanza
Aqabah” maagano haya kwa mujibu wa kumbukumbu za kihistoria yalikuwa ni
katika mwaka wa kumi na mbili (12) wa utume. Qur-ani tukufu imetusajilia
na kutuwekea kumbukumbu za tukio hili lililoleta mapinduzi makubwa katika
historia ya uislamu, tusome pamoja “BILA SHAKA WALE WANAOFUNGAMANA NAWE
KWA HAKIKA WANAFUNGAMANA NA ALLAH, MKONO WA ALLAH UKOO JUU YA MIKONO YAO.
BASI AVUNJAE AHADI (hizi) ANAVUNJA KWA KUIDHURU NAFSI YAKE NA ATEKELEZAYE
ALIYOMUAHIDI ALLAHA (Allaha) ATAMLIPA UJIRA MKUBWA,”(48:10)
Ni
yapi yaliyokuwamo ndani ya maagano/mafungamano haya? Ibn Ishaaq mtaalamu
mashuhuri wa fani ya sira na historia kwa ujumla amepokea ikiwa nai riwaya
itokanayao na Bwna Ubaadah Ibn Swaamit (mmoja wapo wa wanafungamanao)
Amesema: “Tuliagana na Mjumbe wa Allah Rehema na Amani zimshukie ya
kwamba:-
Hatutamshirikisha
Allah na chochote, wala
-
Hatutoiba,
wala
-
Hatutozini,
na wala
-
Hatutawauwas
watoto wetu, wala
-
Hatutaleta
uzushi tunaouzua tu wenyewe, na wala
-
Hatutamuasi
katika jambo jema.
Mtume
akasema kutuambia “Mkiyatekeleza mtapata pepo, na ikiwa mtaghushi
(mtafanya udanganyifu mkavunja) lolote katika (ahadi) hizo (mlizozitoa).
Mtaadhibiwa kwa kupata adabu/adhabu yake (kosa hilo) hapa duniani na hiyo
ndio kafara yake. Ama (mtakapuvunja ahadi) na mkasitiriwa (msijulikane)
mpaka siku ya Qiyamah, basi suala lenu hilo litakuwa katika mikono ya
Mwenyezi Mungu Mtukufu, akitaka ama atakuadhibuni au atakusameheni.”
Watu
wote hawa walisilimu mbelle ya Mtume na kuwa waislamu wema, watiifu na
waaminifu kwa Allha na Mtume wake Ibn Is-haaq Allah amrehemu anazidi
kusema “Walipoondoka watu hawa, Mtume wa Allah Reheme na Amani zimshukie
aliwapa (Swahaba wake) Musw-ab Ibn Umayr na akamuamrisha akawasomesha
Qur-ani, awafundishe uislamu na Fiq-hi ya kiislamu. Akawa Musw-ab akiitwa
(Msomeshaji/mwalimu) katika mji wa madina’
Madinah
mwalimu Musw-ab Ibn Umayr alifikia katika nyumba ya Bwana As-ad Ibn
Zuraarah wa ukoo wa Baniy Najjaar. Huyu ndiye aliyekuwa ukoo wa mwenyeji
wake. Ni vema tukakumbuka kwamba bwana huyu alikuwa ni miongoni mwa watu
wa kabila la Khazraji waliosilimu mbele ya mtume na kuhudhruia maagano
yote mawili. Lile la kwanza la Aqabah na la pili lililofanyika hapo hapo
Aqabah ndugu wawili hawa katika dini wakashirikiana pamoja katika
kuutangaza uislamu Madinah. Walitumia njia ya nasaha na upole katika
kuwakinaisha na kuwashawishi wenyeji wa madinah kuingia katika uislamu.
Ibn
Ishaaq na Ibn Al-athiyr wanasimulia baadhi ya yaliyotukia madinah wakati
alipoingia katika mji huo mwalimu Musw-ab wanasema siku moja Asad Ibn
Zuraarah alitoka na mgeni wake Mwalimu Musw-ab Ibn Umayr, wakingia katika
bustani ya Baniy Dhwafar, watu waliokwishasilimu wakakaa kuwazunguka
Sa’ad Ibn Muaadh na Usayd Ibn Hudhwayr wakasikia juu ya mkutano huu hawa
wakati huo walikuwa ni viongozi wa koo zao na walikuwa ni makafiri, bado
hawajasilimu. Saa’ad akamwambia mwenziwe Usayd “waendee watu wawili
hawa waliokuja majumbani mwetu uwakemee na uwakataze. Kwani lau si As’ad
Ibn Zuraarah ambaye ni mwana wa mama yangu mdogo, ningekutoshea kazi hii.
“baada ya kuambiwa hivyo tu, Usayd akatwaa mkuki wake na kuwaendea
alipofika akawauliza. Ni lipi lililokuleteni, kuwatukana wanyonge wetu?
Tuondokeeni! Mwalimu Musw-ab akamwambia: Hukai kidogo ukasikiliza?
Ukiliridhia tulisemalo likubali, na ukilichukia tutaacha likuchukizalo.
Usayd akasema “Umefanya uadilifu,” akakaa Musw-ab kama mwalimu mzoefu
bila kuchelewa akanza kumpasha juu ya Uislamu, nae akisikiliza kwa makini.
Alipokoma, Usayd akasema: "Habari nzuri na njema zilioje hizi! Hivi
mnafanyaje mnapotaka kuingia katika dini hii? Wakamwambia {Musw-ab na
As-ad}: unakoga na kuzitwaharisha nguo zako, kasha unatoa shahada ya haki,
halafu unaswali rakaa mbili Usayd akayafanya yote hayo na akasilimu kasha
akawaambia hakika nyumba yangu kuna mtu mmoja, huyo akikufuateni hatobakia
nyuma yeyote katika watu wake ila atakufuateni, mtu huyu ni Sa’ad Ibn
Mu’aadh, nami nitamtuma kwenu. Kisha akashika njia kumuendea Bwana
Sa’ad na watu wake. Sa’ad alipomuangalia akasema: Namuapia Mwenyezi
Mungu, hakika Usayd amekujieni na uso mwingine, sio ule aliotoka nao hapa!
Halafu akamuuliza rafiki yake Usayd Hebu niambie kweli, umefanya nini?
Akamjibu Nimezungumza na watu wawili wale, basi wallah! Sikuona ubaya
wowote kwo. Nae yaani Sa’ad akawaendea kama alivyowaendea rafiki yake
akiwa mkali kweli kweli. Akapozwa kwa maneno mazuri kama aliyoambiwa
mtangulizi wake, akalainika na kukaa chini kusikiliza, akasomewa Qurani.
Akaukubali uislamu na kusilimu kasha akarudi kwa jamaa zake akiwa na
rafikiye Usayd Ibn Zuraarah, alipofika akawauliza: Enyi kizazi cha kukoo
wa Abdil ash-hal, mnanitambuaje mimi kwenu? Wakamjibu kwetu wewe ni Bwana
na mbora wetu. Akawaambia Basi ikiwa msemayo ndiyo ni haramu kuanzia sasa
nyinyi kuzungumza na mimi, nyote waume kwa wake mpaka mumuamini Allah na
Mtume wake! Basi baada ya kumaliza kusema hivyo tu hakubakia mwnaamume
wala mwanamke katika jamaa zake ila alisilimu.
Mwalimu
Musw-ab na As’ad wakaendelea kuulingania uislamu Madinah mpaka
haikusalia nyumba yoyote ila walikuwemo humo waislamu wake kwa waume.
Kukawa hakuna kinachozungumzwa Madinah ila ni juu ya Uislamu tu. Hivi
ndivyo yalivyokuwa maagano ya kwanza ya “Aqabah” yaliyokuwa kati ya
Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie na kundi la watu kumi na mbili
kutoka Madinah {Yathrib} Allah awawiye radhi.
|