|
iii.
HIJRAH YA
MTUME KUTOKA MAKKAH KWENDA
MADINAH.
Makurayshi
walifanya kikao chao hiki
kiovu katika mazingira na hali ya uficho na siri kuu ili kuhakikisha kuwa
maamuzi yatakayofikiwa hayavuji na kuwasambaa. Kwani hili halitamaanisha
kingine zaidi ya kushindwa kwa
mpango huu mzima
na hivyo kumpa ushindi Mtume
wa Allah. Lakini Allah mbora wa
kupindua hila za
watu wabaya, mwenye khabari
za lililotendeka linalotendeka na
litakalotendeka kabla hata halijafikiriwa kutendwa bali kabla ya
kuubwa hao watendaji “HAKIKA ALLAH NI MJUZI WA KHABARI ZA SIRI NA
KHABARI ZA DHAHIRI” ( 4.35)
“………NA
ALLAH ANA KHABARI ZA YOTE MNAYOYATEDA”
( 3.153)
Akampelekkea
mtume wake khabari zote za mkutano ule muovu kupitia kwa Allah
imshukuru – na akampa idhini ya kuhamia Madina. Sasa ndio Bwana
Mtume akaanza kupanga mikakati ya Hijrah kwa hadhari
kubwa ili asiwashitue
Makurayshi. Mtume akatambua
kwamba Makurayshi wataizingira nyumba yake
usiku ili kumzibia
mwanya wa kutoroka. Iwapo atafanikiwa kutoroka basi ni dhahiri kuwa
wataanzisha msako wa nyumba
hadi nyumba Makkah nzima, wakimkosa watamtafuta katika njia ielekeayo
Madinah wataziba njia zote za kutoka Makkah ili ashindwe kutoka nje, na
watafanya juhudi za makusudi
ili waweze kumtia mikononi. Wakishindwa
kumkamata kwa mbinu zoote hizo , basi bila ya shaka watakataa
tamaa na kuinua mikono ya kushindwa
na hapo ndipo hali
itarejea kuwa ya kawaida
mjini Makkah.
Ni
kuanzia hapo ndipo Mtume wa Allah rehema na Amani zimshukie – aakaanza
kupanga mikakati yake
ya kuondoka Makkah . Akamuendea Aliy Ibn Abiny Twaalib: mwana wa Ammi
yake na kumuelezea juu ya
azma yake ya kuhama na akamtaka aendelee
kubakia Makkah ili aweze kurejesha
amana zaa watu walizomuwekea yeye mtume kwani watu
wa Makkah walikuwa wakiweka kwa
Bwanaa Mtume
amana zao na vitu vyao
vingine vya thamani kutokana na kuutambua ukweli na uaminifu wake. Kisha
huyo haraka akatoka
mguu mosi mguu pili mpaka
nyumbani kwa Swahibu
yake Abuu Bakri – Allah amuwiye radhi
ili ampe khabari ya Hijrah . Pia
amuelezee kwamba yeye
ndiye rafiki mteule katika saafari hii yake
ya hijrah. Kisha wapange na kuwafikianna
pamoja namna na wakati wa
kutoka ili safari yao usikumbanne na
vikwazo vya makurayshi.
Tumpe nafasi Ibn Ishaaq –
Allah amrehemu – aripoti kutoka kwa
Bi. Ayshaa mkewe Mtume
akisimulia namna mambo
yalivyokuwa , anasema {
Bi Aysha} : “ Yalikuwa si mazoea ya
Mtume wa Allah – Rehema na Amani
zimshukie - kuja nyumbani kwa
Abuu Bakri {baba yangu }
katika mojawapo ya
ncha mbili
za mchana {Adhuhuri na laasiri } Bali alikuwa akija
ima asubuhi au Jioni. Hata ilipofika ile siku ambayo Allah alimpa
idhini ya kuhama Mtume wake . Atoke Makkah machoni mwa jamaa zake ,
alitujia mtume wa Allah rehema
na Amani zimshukie – wakati
wa jua kali la mchana , katika muda
ambao hakuuzoea . {Anasema ni kumwambia : Hakuja
Mtume wa allah saa
hizi ila
kuna jambo tu lilitokea { Akaendelea kusema
Bi. Aysha} Alipoingia,
Abuu Bakri akampisha kwenye
godoro lake , Mtume akakaa. Hakuwepo mtu mbele
ya Abuu Bakri ila mimi na
dada yangu Asmaa. Mtume wa Allah
akasema "Niondoshee walioko pamoja nawe" Akasema Abubakri
"Ewe Mtume wa Allah, hakika hawa
si watu baki ila ni mabinti zangu , kwani kuna jambo
gani?" {Mtume} akamwambia “ Hakika Allah amenipa idhini ya
kutoka na kuhama". {Anasema Bi Aysha} Abu Bakri akasema :
"Tufuatane pamoja
ewe mtume wa Allah” {
Mtume} akamjibu : “ Tutafuatana pamoja
“ { Anaendelea kusema
Bi. Aysha } Wallah sikuhisi wala kujua kabla ya siku hiyo kwamba
mtu anaaweza kulia kwa furaha mpaka nilipomuona
Abu Bakri siku hiyo akilia, kisha
akasema “ Ewe Mtume
wa Allah hakika vipando {wa nyama }
viwili nilikuwa nimeviandaa tayari kwa ajili ya safari hii”
Wakamkodi Abdullah Ibn
Urayqitu, mtu wa kabila
la Banny Duili aliyekuwa kafiri, afanye kazi
ya kuwaongoza njia. Wakampa wanyama wawili wale
akae nao na kuwachunga mpaka siku
ya safari “ Amemalizaa kuripoti
Ibn Is-Haaq.
Mpango
waliopanga Mtume wa Allah Rehema na Amani zimshukie na swahibu
yake Abu Bakri ni
Kutoka Makkah usiku na kwenda mpaka
katika pango la “Tha uri” nje kidogo ya mji wa Makkah.
Wajifiche hapo kwa muda mpaka tafrani
ya kuwatafuta itulie kabisa . Kisha ndipo
watoke na kuelekea na watu. Hivi ndivyo ulivyokuwa
mpango mzima wa safari ya Mtume na
Swahibu yake kuhamia Madinah , kwenda kuungana na
maswala wake watu waliomkubali kwa dhati
na kumtafuata kwa nia.
Wakaagana na Abdullah Ibn
urayqit; mtaalamu wa njia za
jangwani awafuate kati mtaalamu
wa njia za jangwani awafuate
katika pango la
thauri baada ya siku
tatu watakapotoka.
Wasifu
wa Pango “ Thauri”
Thauri,
hili ni pango lililopo juu ya
jabali Thauri, huu ni mlima mrefu wenye
vilele viwili . Mlima huu uko
umbali wa maili tatu kusini mwa
mji wa Makkah katika njia ielekayo
nchi ya Yemen . Kutoka mjini Makkah mpaka katika pango
hili ni mwendo wa
masaa mawili kwa
miguu. Pango hili liko
kileleni mwa mlima
huu. Ni pango finyu
lenye eneo lisilozidi mita
mbili na nusu. Limelala chini ya mwamba
mkubwa ambao unakuwa
mithili ya paa linalilifanya
pango hili
kuwa na kiza
cha kutisha . Pango hili kuwa
na kiza cha kutisha. Pamoja
hili lina penyenye
mbili zinazopatikana kwa taabu kila upande, hii ndio
milango ya pango hili.
Hili ndilo pango alilijificha
ndani yake Mtume wa Allah na Swahibu yake kwa muda wa siku tatu na hayo
ndiyo mazingira yake. Kwa wale
watakaojaaliwa kufika katika mji mtukufu wa Makkah wanaweza kuliona pango
hili.
Usiku
ule
Hatimaye
ukafika ule usiku uliokuwa
ukisububiriwa kwa hamu na kiu kubwa sana. Bwana
Mtume akiusubiri ili aweze kuitekeleza amri ya Mola wake yaa
kuhamia Madinah. Nao makurayshi kwa upande
wao wakiusubiri ili waweze kuitekeleza azma yao ya
kummaliza mtume wa
Allah na dini yake ambayo ni
tishio kwa itikadi yao ya ushirikina.
Usiku ule wale
vijana shujaa ,
barabara wenye nguvu na wenye
nia moja , wakiwa na panga
kali waliizingira nyumba ya
Mtume . Wakimsubiri atoke
tu, waitekeza kazi
na jukumu walilopewa na
desturi ya Waarabu kumuua mtu ndani
ya nyumba yake. Ally Ibn Abiy
Twaalib akalala katika kitanda cha Mtume kama
alivyoelekezwa na akajifunika shuka la kihadharami la rangi ya kijani la
Mtume . Ikumbukwe wakati wote
huu, Bwana Mtume alikuwa
angali ndani . Ulipowadia
wakati wa
kutoka allah akawashushia
usingizi wa ajabu vijana wale walioizunguka nyumba ya Bwana Mtume .
Wakalala nao wakiwaa hawajitambui kwa usingizi . Akachukua mchanga
akawanyunyuzia wote vichwani
huku akisoma mwanzo mwanzo wa
Suwarati Yaasin: NA{ Kama kwamba}
TUMEWEKA KIZUIZI
MBELE YAO NA KIZUIZI NYUMA YAO NA TUMEWAFUNIKA { MACHO
YAO} KWA HIYO HAWAONI
‘ { 36;9}
Huyoo
akashika njia , akakutana na Sayyidna Abuu Bakri Mahala walipoagana
kukutana . Wakaongozana mpaka katika
pango la Thauri na kujificha
humo. Huku nyuma , Kulipombazuka
asubuhi , vijana wale
wakamuona Ally ndiye anaamka kitandani kwa Mtume
. hapo ndipo wakachanganyikiwa na kupandwa na mori
wa hasira . Wakamnyakua Sayyidna Aliy , wa kimsukasuka huku na kule
wakimuuliza : Yu wapi Muhammad?
Ameenda wapi? Amejificha wapi Nae
Imam Ally akiwajibu kwa
utulivu na makini:
“ Sijui mmemshurutiza kutoka nae ametoka
” Wakaanza
kumpiga , kisha wakamchukua mpaka
msikitini wakamfungia humo. Wakamkusanyikia na kutumia kila
njia ili aweze kusema alipo Mtume
lakini wapi hakusema .
Walipokata tamaa walimuachia
na wakatawanyika pande zote za Makkaah kuanza kumsaka Bwana Mtume
kwa bidii zote. Wakaenda Mashariki
na Magharibi, Kaskazini na Kusini, huku wakimuuliza kila
waliyekutana naye njia
. Lakini juhudi zote hizi hazikuzaa matunda.
Amepokea
Ibn Is Haq – Allah amrehemu – kutoka kwa Bi Asma Bint Abiu Bakri
kwamba yeye { Asma } amesema
{ Katika kuelezea hali iliyokuwa} “
Alipoondoka Mtume wa Allah
– Rehema na Amani zimshukiee – na
Abuu Bakri – Allah amuwiye radhi – lilitujia kundi la
Makurayshi akiwemo Abu Jaahli Ibn Hishaam. Wakasimaama mlangoni mwa nyumba
ya Abuu Bakri , Nikawatokea ,
wakaniuliza : yu wapi babayo awe bint Abuu Bakri? Akasema
Bi Asmaa} Nikaawajibu : Wallah ! sijui baba yangu yuko wapi. {
Akaendelea kusema}: Abu Jahli akainua mkono wake na alikuwa mtu muovu
mwenye maneno machafu, akanipiga kofi la nguvu lililo zidondosha chini
hereni zangu.
Mtume
na Swahibu pangoni:
Mtume
wa Allah – Rehema na Amani zimshukie yeye na swahibu yake wakakaa
pangoni mle kwa muda wa siku tatu. Wakisikiliza khabari za vuguvugu la
kumtafuta. Ibin Is–haaq anasema: “Abdullah Ibn Bakri alikuwa akishinda
na Makurayshi mchana kutwa akisikiliza mikakati wanayopanga ili kuweza
kuwatia mbaroni Bwana Mtume na swahibu yake. Kisha jioni huenda pangoni
kuwapasha khabari. Aamir Ibn Fuhayran – huru wa Abuu Bakri – yeye
alikuwa akichunga mchana katika machungo ya watu wa Makkah. Jua likichwa
huwapeleka mbuzi wa Abuu Bakri kule pangoni, wakawamua maziwa na kumchinja
mmoja wakala nyama Abdullah Ibin Abuu Bakri akiondoka kule pangoni kurudi
Makkah, Aamir Ibin Fuhartah alimfuatia nyuma na mbuuzi ili kuziba / kufuta
athariya miguu yake. Baada ya kupita siku tatu, mtu wao waliyemuajiri
akaja na ngamia wao na ngamia wake yeye tayari kwa safari”
Pamoja
na ugumu wa kipindi hiki cha kutoka Makkah hadi pangoni Thauri na maisha
ya pangoni mle bado Mtume alikuwa na imani thabiti juu ya ulinzi
usionshindikana wa mola wake. Hasa pale vijana wa Kikurayshi walipotumia
uhodari wa kufuatilia nyayo za watu mpaka wakafika pangoni pale. Na Abuu
Bakri akawa anasikia sauti zao na mchakacho wa miguu yao. Khofu ikamtambaa
Abuu Bakri, akaanza kulia ka kuona kuwa sasa maisha ya Mtume wa Allah yamo
hatarini. Akasema “Ewe Mtume wa Allah, lau mmoja wao ataangalia chini ya
miguu yake, bila shaka watatuona Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie
– akafanya kazi ya kumtuliza Abuu Bakri na akamwambia :” Usihuzunike
hakika Allah yu pamoja nasi! Unawadhaniaje wawili ambao Allah ni watatu
wao?” Bukhaariy Muslim.
Qur
– ani tukufu ametusajilia tukio hillo, tufuatane nayo: “KAMA
HAMTAMNUSURU {Mtume} BASI ALLAH ALIMNUSURU WALIPOMTOA WALE WALIOKUFURU;
ALIPOKUWA {mmoja tu na
mwenziwe} wa Pili wake {peke yao} WALIPOKUWA WOTE WAWILI KATIKA PANGO ;
(Mtume) ALIPOMWAMBIA SWAHIBU YAKE : “ USIHUZUNIKE KWA YAKINI ALLAH YU
PAMOJA NASI ;ALLAH AKAMTEREMSHIA UTULIVU WAKE NA AKAMNUSURU KWA MAJESHI
MSIOYOYAONA (9: 40)
Majeshi
aliyoyatumia Allah kumuhami, kumlinda
na kumnusuru Mtume wake dhidi ya maadui hawa
wenye uchu na kiu ya kumuua ni yule mdudu
buibui aliyekuja akautanda utandu wake mlangoni mwa pango kwa Il-ham
ya Allah. Halafu akaja ndege
akataga mayai pale .
Makurayshi walipofuata nyayo na kufika
pangoni walikataa katakata
kuwa Mtume yumo pangoni mle wakasema . Haiwezekani aingie pangoni humu
bila ya kuvunja mayai haya na kuuharibu utandu huu. Hao
wakashika njia na kwenda zao. Baada ya kupita siku tatu ,
Makurayshi walikata tamaa kumpata Mtume
Makkah. Wakaamua kuzielekeza juhudi na nguvu zao. Katika njia kuu
ulekeayo Madinah. Wakawatuma huko vijana wao kuendelea kumsaka Mtume wa
Allah . Wakawatangazia wakazi wote wa Pwani kwamba yeyote atakayemleta
Mtume akiwa hai au amekufa
atazawadiwa zawadi nono ya ngamia mia.
Habari zote hizi zikimfikia Bwana Mtumee kupitia kwa Abdallah Ibn
Abuu Bakri na akazitumia kamma chanzo cha kupangia
mkakati wa kutoka
pangoni mle na kuanza safari ya Madinah.
|