|
Imetubainikia bayana
katika somo lililotangulia kwamba makurayshi katika upinzani wao wa mtume
walikuwa hawaitetei imani yao bali walikuwa wakijaribu kulinda utawala wao na
maslahi yao na hatari hii ya kuanguka kwa utawala wao na kuporomoka kwa
maslahi yao ndio iliyokwasukuma kuingia mapambanoni dhidi ya uislamu wao na
kiongozi wake wakajaribu kwa nguvu zao zote kumdhibiti Bwana Mtume asitoke nje
ya mpaka ya Makkah kwa hofu kuenea na kutapakaa uislamu ambao waliuona kama
tishio kuu kwa utawala wa maslahi yao pamoja na udhibiti huu bado Uislamu
ulifanikiwa na kupenya na kuingia Madinah, huko ukaenziwa na kupata watu walio
tayari kulinda kutetea na kunusuru hata kwa gharama ya roho zao. Kuingia
uislamu kwa madinah kwa kishindo kikubwa kilibadili kabisa sura ya Madinah
kutoka nchi fulani jirani rafiki na mshirika wa Makkah kuwa nchi tishio na
adui mkubwa wa Makurayshi. Makurayshi waliona hatari hii inayochungulia na
wakaamua kuchukua hatua haraka za makusudi ili kukabiliana na hatari hii iliyo
mbele ya macho wakaamua na kuazimia kumuua kiongozi wa hatari hiyo Bwana Mtume
kabla hajainua mguu kuhamia Madinah na kwenda kuzidisha hali ya hatari
inayowakabili kwani waliamini kuwa yeye ndiye kiongozi na chimbuko la vuguvugu
la Uislamu. Makurayshi walisahau kuwa Muhammad alikuwa ni mjumbe tu wa Allah
na mmiliki wa Uislamu ni Allah. Kwa hiyo kuumua kwao Bwana Mtume
hakutaamanisha kufa kwa Uislamu kama dini na mfumo sahihi wa maisha uliofumwa
na Allah. tusome na tuone ukweli: YEYE NDIYE ALIMLETA MTUME WAKE KA UONGOZI NA
DINI YA HAKI ILI AIJALIYE KUISHINDA (dini hiyo) DINI ZOTE ITAPOKUWA
WANAICHUKIA HAO WASHIRIKA". (9:33)
Kadhalika walisahau kuwa
Mtume hawezi kuuwawa kwani ana ahdi ya Allah ya kumlinda dhidi ya maadui wa
da'awah:".... NA ALLAH ATAKULINDA NA WATU..." (5:67)
Ni kutokana na ahdi hii
ndiyo Allah akamuondoshea Mtume wake rehma na amani zimshukie vitimbi na njama
zote za maadui wa haki na uongofu. Akamuandalia njia ya Hijrah kwenda Madinah
na huko akamujengea na kumuwekea mazingira yote yaliyohitajika kwa ajili ya
maendeleo na ustawi wa da'awah.
MAKURAYSHI WALIENDELEA
KUPIGA VITA UISLAMU MADINAH KAMA WALIVYOKUA WAKIPIGA VITA MAKKAH
Tayari
imeshatudhihirikia kwamba Hijrah ya Mtume -Rehema na amani zimshukie –haikuwa
ni kuisalimisha nafsi yake asiuliwe na Makurayshi. Wangeweza vipi kumuua hali
ya kuwa ulinzi wa Allah mshindi mwenye nguvu pamoja nae kila alipo? ni dhahiri
basi Hijrah haikuwa ila kwa ajili ya da'awah, ni kwa ajili ya kupata kituo cha
da'awah. Ni kwa ajili ya kupata mazingira mazuri yatakayomuezesha kulitekeleza
vema jukumu alilopewa na mola wake. Jukumu la kusimika Uislamu ulimwenguni
kote ili watu waishi kwa furaha, amani, upendo usawa na haki, ichukue nafsi ya
dhulma.
Haikuingia akilini
makurayshi wamnyamazie Mtume na kumuacha aishi kwa amani na akieneza Uislamu
kama apendavyo, kwani kufanikiwa na kuenea kwa Uislamu maana yake ni kufa kwa
muhimili wa utawala wa maslahi yao. Vipi basi yawezekana wamuachie atulizane
Madinah na kuzidi kuyahatarisha maslahi na utawala wao? Gharama zote za
mapambano na upinzani mkali wa Makkah zipotee bure bure tu, eti kwa sababu tu
yuko Madinah ! Hata haiwezekani kuwachiwa hivi hivi tu wakati tayari
amekwishaonekana kuwa ni hatari na kikwazo kwa misafara yao ya biashara ya
kutoka na na kwenda nchi za kaskazini. Mji wa Madinah ulikuwa ni njia kuu za
misafara hii. Kwa mtazamo huu kulikuwa hakuna shaka kwamba Makurayshi
watarudufisha juhudi zao katika kupambana na Uislamu ili kulinda maslahi zo na
utawala wao na watafanya kila lililo katika uwezo kuwashawishi warabu wengine
wajiunge nao katika kukabiliana na hatari hii (Uislamu) na hatimaye
kuitokomeza kabisa. Na hizo ndizo hatua zilizochukuliwa na Makurayshi, kwani
tangu wakati huo walianzisha juhudi za makusudi za kueleza ubaya na hatari za
Uislamu. Walipeleka ujumbe wao maalumu katika makabila ya mayahudi yaliyokiua
yakiishi nje ya Madinah kwa lengo la kujenga chuki baina yao na waislamu.
Kutokana na juhudi hizi mbaya, waislamu waliishi kwa khofu na tahadhari kubwa
katika siku za mwanzo za maisha mapya ya Madinah wakitazamia mashambulizi
wakati wowote kutoka kwa adui aliye nje ya mipaka yao na ndani.
MAKURAYSHI HAWAKUWA
ADUI PEKEE WA VUGUVUGU NA HARAKATI ZA UISLAMU
Je makurayshi ndio
walikuwa maadui pekee wa Uislamu wanaochukua juhudi za makusudi kuupinga n
kuuzuia? La hasha Makurayshi hawakua ndio maadui pekee au wapinzani pekee,
japokuwa wao ndio waliokuwa wa mwanzo kuonyesha chuki, uadui na upinzani.
Ukweli ni kwamba makundi adui mengine mengi na haya ndio makurayshi walijaribu
kuyakusanya na kuyaunganisha pamoja ili kuwa na upinzani mkali na wenye nguvu
utakaorahisisha kuutokomeza Uislamu na kuumua Mtume wa Allah. Makundi haya
yalijumuisha mayahudi wengi wa Madinah na wale walioishi nje ya Madinah.
Yalikuwepo pia makundi ya wanafiki ndani ya Madinah kwenyewe na pembezoni
mwake kama yalivyokuwepo makundi ya washirikina wenyeji wa Madinah na
mushirikina wa makabila mengine ya waarabu. Aya ifuatayo inadhihirisha baadhi
ya makundi hayo: “NA KATIKA MAADUI WANAOKAA PEMBEZONI MWENU KATIKA VITONGOJI
VYA KARIBU YENU (hapo madinah) KUNA WANAFIKI NA KATIKA WENYEJI WA MADINAH (pia
kuna wengine wanafiki) WAMEBOBEA KATIKA UNAFIKI (hata) HUWAJUI (kuwa ni
wanafiki) SISI TUNWAJUA TUTAWAADHIBU MARA MBILI (mara ya kwanza kwa majanga na
fedheha na ya pili wakati wa kufa) KISHA WATARUDISHWA KATIKA ADHABU KUBWA"
(9:101)
Makundi yote haya
yalikuwa ni maadui dhahiri wa da’awah ya Uislamu, yalifanya kila juhudi
kuhakikisha kuwa Uislamu unatokomezwa kabisa katika uso wa ardhi : “…
LAKINI ALLAH AMEKATAA ISIPOKUWA KUITIMIZA NURU YAKE (Uislamu) IJAPOKUWA
MAKAFIRI WANACHUKIA” [9:32].
Katika upinzani na vita
hivi, makundi haya adui yaligawika kimalengo. Kuna makundi ambayo lengo
lililowasukuma katika mapambano huu ilikuwa ni kulinda utawala na maslahi yao
yasiporwe na mfumo mpya wa maisha (Uislamu). Kuna ambayo yalijitumbukiza
vitani kwa chuki kongwe binafsi za kurithi kizazi hata kizazi. Mengine
yalijikuta yakiingia mapambanoni kutokana na ushawishi wa washirika na
marafiki zao. Kadhalika yako makundi yaliyosukumwa vitani kwa hasadi na chuki
ya Imani, kundi hili ndilo Allah analitaja katika kitabu chake : “WENGI
MIONGONI MWA WATU WALIOPEWA KITABU (Mayahudi) WANAPENDA WANGEKURUDISHENI
NYINYI MUWE MAKAFIRI BAADA YA KUAMINI KWENU, KWA SABABU YA HUSUDA ILIYOMO
MOYONI MWAO (iliyowapata) BAADA YA KUWAPAMBANUKIA HAKI …” [2:109]
MAYAHUDI WALIOPINGA
UISLAMU KWA HUSDA NA MAYA
Imekwishatubainikia
kwamba Makurayshi waliona Uislamu kuwa ni tishio kwa maslahi yake, hivyo
walipambana nao kwa nguvu zote kwa sababu kutetea masahi yao na kulinda
utawala wao. Ama Mayahudi hili lilikua ni kundi lililoelemika lina mabaki ya
mafundisho sahihi ya mbinguni. Walikuwa ni Ahlul-Kitaab walivyoita na Qurani
mahala pengi: “ENYI WATU MLIOPEWA KITABU (cha Allah, mayahudi na manasara)
NJOONI KATIKA NENO LILILO SAWA BAINA YETU NA BAINA YENU; YA KWAMBA TUSIMUABUDU
YOYTE ILA ALLAH WLA TUSIMSHIRIKISHE NA CHOCHOTE……." (3:64)
Kutokana na elimu ya
kitabu walivyokua nayo mayahudi ndio walitazamiwa kua watu wa mwanzo kuamini
Mtume wa Allah na risala yake hii ni kwa sababu kitabu chao kilikua nikanatoa
bishara ya ujio wa Nabii Muhammad sifa zake na mahali atakapoondokea. Tena
sababu ya kuja mtume haya yameelezwa wazi kua kuikamilisha taurati waliyopewa
na si kuitangua: "ENYI KIZAZI CHA ISRAEL (Nabii Yakub yaani enyi Mayahudi)
ZIKUMBUKENI NEEMA ZANGU NILIZOKUPENI NA TEKELEZENI AHADI YANGU (ya kua akija
Mtume mtamufata) NITATEKELEZA AHADI YENU (ya kukupeni pepo) NA NIOGOPENI MIMI
TU NA AMININI NILIYOYATERREMSHA AMBAYO YANASADIKISHA YALIYO PAMOJA NANYI WALA
MSIWE WA KWANZA KUKATAA…"(2:40-41)
Lakini kwa bahati mbaya
Mayahudi pamoja na kutambua ukweli bado hawakua tayari kuukiri kwa sababu ya
kutawaliwa na maumbile ya uchoyo na ubinafsi. Mitume wengi walitoka katika
utaifa wa israel kwa nini huyu mtume asitoke kwao na atoke kwa ndugu zao
waarabu ? Mtume huyu kuwa mwarabu nasi myahudi ni ishara ya wazi kuwa utume na
utukufu unahama kwao na kwenda kwa waarabu. Mayahudi waliitakidi kwamba wao
ndio wana wa Mungu wapenzi wake na taifa lake teule na mantiki hii Mtume
hawezi kutoka nje ya taifa yao: NA MAYAHUDI NA MANASARA WANASEMA SISI NI WANA
WA ALLAH NA WAPENZI WAKE" SEMA: BASI KWANINI ANAKUADHIBUNI KWA AJILI YA
DHAMBI ZENU? BALI NYINYI WATU KATIKA ALIWOWAUMBA….." (5:18)
Allah alipopeleka Mtume
kutoka kwa waarabu na si mayahudi nyoyo zao zilijaa chuki na ghera
zikaunguliwa kwa hasadi na mfundo. Wakaanza kuhoji na kutilia shaka utume na
dini yake wakawa wanasema huyu Muhammad siye mtume ambaye tuliyekuwa
tunamtazamia na kungojea. Wakayachoma moto maandiko matakatifu yaliyomo katika
kitabu chao yanayomhusu na kumtaja Nabii Muhammad wakabadilisha maandiko yote
yanayomtaja jina au wasifu na Mtume huyu na wakaanza kumchukia kumfanyia uadui
na kusema: ALLAH AMETUAHIDI YA KUWA TUSIMUAMINI MTUME YEYOTE MPAKA ATULETEE
KAFARA MBAYO HULIWA NA MOTO…." (3:183)
Walikusudia kumfanya
mtume ashindwe na hivyo kubatilisha utume wake. Wakaongozwa na hasadi hii
kuupiga vita uislamu kwa nguvu zao zote mpaka kudhihiri katika uso wa ardhi
dini nyingine ila dini yao tu.
Mtume aliutambua uadui
huu lakini pamoja na hayo aliwalingania Uislamu kwa upole, ulaini na hoja,
akiwambia : “ENYI WATU MLIOPEWA KITABU (cha Allah, Mayahudi na Manswara)!
NJOONI KATIKA NENO LILILO SAWA BAINA YETU NA AINA YENU; YA KWAMBA MUISIMUABUDU
YEYOTE ILA ALLAH, WALA TUSIMSHIRIKISHE NA CHO CHOTE, WALA BAADHI YETU
TUSIWAFANYE WENGINE KUWA WAUNGU BADALA YA ALLAH …” [3:64]. Na akiwasuta
kwa upole na ulaini pia : “SEMA : ENYI WATU MLIOPEWA KITABU ! KWA NINI
MNZAIKATAA HOJA ZA ALLAH, HALI ALLAH NI SHAHIDI JUU YA YOTE MNAYOTDENDA ? SEMA
: ENYI MLIOPEWA KITABU! KWANINI MNAWAZUILIA (watu) NA NJIA (dini) YA ALLAH
WALE WALIOAMINI ? MKAITAFUTIA KOSA, NA HALI MNASHUHUDIA (kuwa ni njia ya Allah
isiyokuwa na kosa ) NA ALLAH SI MWENYE KUGHAFILIKA NA MNAYOTENDA “
[3:98-99]. Na akiwakumbusha neema ya Allah juu yao na wito wake kwao : “ENYI
KIZAZI CHA ISRAILI (Nabii Yaaqub ! Yaani Enyi Mayahudi !) ZIKUMBKENI NEEMA
ZANGU NILZOKUNEEMESHENI; NA TEKELEZENI AHADI YANGU (ya kuwa akija Mtume
mtamfuata) NITAITEKELEZA AHADI YENU (ya kukupeni pepo) NA NIOGOPENI MIMI TU.
NA AMININI NILIYOYATEREMSHA AMBAYO YANASADIKISHA YALIYO PAMOJA NANYI, WALA
MSIWE WA KWANZA KUYAKATAA. WALA MSIYAUZE MANENO YANGU KWA AJILI YA THAMANI
NDOGO TU (ya kilimwengu) NA NIOGOPENI MIMI TU. WALA MSICHANGANYE HAKI NA
BATILI, NA MKAFICHA HAKI NA HALI MNAJUA. NA SIMAMISHENI SWALA (Enyi Mayahudi)
NA TOENI ZAKA NA INAMENI PAMOJA NA WANAOINAMA (yaani kuweni Waislamu) JE,
MNAWAAMRISHA WATU KUTENDA MEMA NA MNAJISAHAU NAFSI ZENU, HALI MNASOMA KITABU (cha
Allah kuwa kufanya hivyo ni vibaya) ? BASI JE, HAMFAHAMU ?” [2:40-44].
|