|
Miongoni mwa watu waliokuwa mbele ya mpishi wa fitna hii iliyokurubia kuwagawa
waislamu kwa misingi ya Umakkah na Umadinah. Alikuwa ni kijana mdogo ambaye
bado hajafikilia baleghe; Zayd Ibn Arqam, huyu akaichukua khabari ile ya
maneno ya Abdullah Ibn Ubayyi na kumfikishia Mtume wa Allah-Rehema na Amani
zimshukie. Akampasha khabari hiyo akiwa pamoja na kundi la watu kadhaa katika
Muhajirina na Answari. Pale pale uso wa Mtume wa Allah ukabadilika na kusema:
“Ewe kijana huenda wewe una chuki nae?” Akajibu: “Wallah, hapana kwa yakini
nimemsikia”. Mtume akazidi kumuhoji: “Huenda masikio yako hayakusikia vizuri”,
akajibu: “Hapana, ewe Mtume wa Allah!” Akamuuliza tena ili kupata ithibati:
“Huenda umechanganya maneno kutokana na kutatizwa”. Akajibu: “Wallah hapana,
kwa yakini nimemsikia akisema ewe Mtume wa Allah!” Basi yakatangaa na kuenea
kambi nzima maneno aliyoyasema Ibn Ubayyi mpaka ikafikia watu hawana kingine
cha kuzungumzia ila maneno hayo. Sayyidina Umar Ibn Al-Khatwaab akasema: “Ewe
Mtume wa Allah! Muamuru Abaad Ibn Bishri amuulie mbali muovu huyu”. Mtume wa
Allah-Rehema na Amani zimshukie-akamwambia: “Itakuwaje ewe Umar, pale watu
watakapo zungumza ya kwamba Muhammad anawaua maswahaba wake mwenyewe! Hapana
asiuliwe, lakini uidhinishe msafara uanze kuondoka kwa safari ya kurejea
Madinah”. Na huu ulikuwa ni wakati ambao Mtume wa Allah-Rehema na Amani
zimshukie-hakuwa na mazoea ya kusafiri ndani yake; wakati wa jua kali mno.
Khabari ya
kwamba maneno aliyoyasema tayari yameshamfikia Bwana Mtume ikagonga ngoma za
masikio ya msemaji; Ibn Ubayyi. Nae akakanusha na kupinga vikali tena kwa
kumuapia Allah mbele ya Mtume ya kwamba hakusema cho chote, bali anasingiziwa
tu. Bwana Mtume hakumjibu wala kumuuliza lo lote, bali aliendela na safari
yake. Ibn Is-haq-Allah amrehemu-anasema: (Mtume wa Allah-Rehema na Amani
zimshukie-alipokuwa njiani akakutana na Usayd Ibn Hudhwayr, huyu akamuamkia
kwa maamkizi ya utume, kisha akasema: “Ewe Mtume wa Allah! Wallah, kwa yakini
umesafiri katika wakati mbaya ambao hukupatapo kamwe kufunga safari ndani
yake!” Mtume wa Allah-Rehema na |