|
I.
Usaliti na uvunjaji ahadi wa Baniy Quraydhwah ndio upenyo waliopitia
waislamu (ndio sababu ya vita hivi).
Hapana shaka kwamba msaada wa ki-Mungu ndio uliowaokoa waislamu katika vita
hivi vya Ahzaab na kwamba lau si kuja kwa msaada huu, kumalizwa kwa waislamu
lingekuwa ni jambo lisilozuilika. Na da’awah ya Kiislamu ingelifikia ukomo
bila ya shaka na hili ndilo alilokuwa akilichelea Mtume wa Allah-Rehema na
Amani zimshukie. Akawa anamuomba Mola wake pale aliposema: “Ewe Mola wa
haki wee! Ukitaka hutoabudiwa”. Naam, lau Allah angetaka waislamu
washindwe katika vita hivi, Uislamu ungekuwa ni kitu kisichotajikana tena. Na
kingeliangamia kikundi hiki kidogo kilichokuwa kinampwekesha Allah kwa
kumuabudu yeye peke yake bila ya kumshirikisha na ye yote/cho chote sambamba
na kuisimamisha dini yake katika ardhi.
Na
ni jambo lisilokubali mabishano kwamba usaliti na uvunjaji ahadi wa Baniy
Quraydhwah ndio upenyo waliopitia waislamu. Yaani ndio sababu pekee
iliyowahalalishia waislamu kuingia vitani na Mayahudi hawa wa
Kibaniy-Quraydhwah. Lau si usaliti wao huu, mushrikina wasingeliweza kupata
njia ya kuwafikia waislamu, kwani walisimama mbele ya handaki kwa muda mrefu.
Wakalizunguka mara nyingi na wakajaribu mara kadhaa kupata upenyo
watakaopenyea kuwafikia waislamu. Lakini wapi, waislamu walikuwa macho na
makini katika ulinzi kiasi cha kuweza kuziba mianya yote na kuzima majaribio
yote ya kupenyea upande wao. Lilikuwa ni jambo jaizi kwa mushrikina hawa
kukimwa na hali hii na kuchoshwa kusimama mbele ya handaki. Na kukata tamaa ya
kuifikia kambi ya waislamu baada ya kushindwa kwa majaribio yao kadhaa. Uchovu
huu na kukimwa huku ilikuwa ni sababu tosha ya kuwarejesha makwao bila ya
kuyafikia matakwa yao dhidi ya waislamu kama ilivyokuwa shabaha yao. Lakini
kujiingiza kwa Baniy Quraydhwah upande wa majeshi shirika (Ahzaab) na uvunjaji
wao wa ahadi walioahidiana na waislamu. Hapana shaka ndio sababu
iliyowarejeshea mushrikina matumaini mapya baada ya kukata tamaa, kuamsha mori,
kuzidisha ari yao na mbinyo upande wa kambi ya waislamu kiasi cha kuwaendesha
mbio. Hii ndio ikawa sababu kuu ya mtetemesho na khofu iliyowasibu waislamu na
kizaizai kilichotokea katika safu zao. Na ndio iliyowafanya wanafiki na wenye
maradhi mioyoni mwao kuitumia fursa hiyo kuwakatisha tamaa waumini, wakisema
kama walivyonukuliwa na Allah: “...ENYI WENYEJI WA YATHRIBU (Madinah)! HAMNA
MAHALI PA KUKAA NYINYI, BASI RUDINI (makwenu msiingie katika jeshi pamoja na
Muhammad). NA KUNDI JINGINE MIONGONI MWAO LIKAOMBA RUHUSA KWA MTUME KWA KUSEMA:
HAKIKA NYUMBA ZETU NI TUPU (hapana watu, tunakwenda zetu), LAKINI HAZIKUWA
TUPU, HAWAKUTAKA ILA KUKIMBIA TU”. [33:13]
Hakika
wasifu uliotolewa na Qur-ani Tukufu katika kuielezea hali ya waumini katika
mazingira haya magumu, unasawirisha kwa uwazi kabisa nguvu ya hujuma malizi
iliyoelekezwa na mushrikina upande wa waumini. Pale walipowajia kuwashambulia
kutokea juu na chini yao na inaonyesha wazi kiwango cha khofu iliyowapata
waislamu hata macho yakakodoka na nyoyo zikapanda kooni na wakamdhania Allah
dhana mbalimbali: “HAPO WAUMINI WALITIWA MTIHANI (kweli kweli) NA
WAKATETEMESHWA KWA MATETEMESHO MAKALI”. [33:11]
Ulikuwa
ni usaliti na khiana pamoja:
Usaliti huu
uliokurubia kuifagilia mbali dola ya Kiislamu, haukuwa na sababu yo yote zaidi
ya chuki na mfundo vilivyo kuwemo nafsini mwa Mayahudi dhidi ya Waislamu.
Waislamu waliendelea kuwa wakweli na watekelezaji wa ahadi yao waliofunga na
Baniy Quraydhwah. Utekelezaji na ukweli huu kwa ahadi yao ukawa ndio hoja kuu
aliyoitumia Ka’ab Ibn Asad kwa Huyay Ibn Akhtwab pale alipokuwa akijaribu
kumshawishi kuvunja ahadi na Mtume, alipomwambia: “Ole wako ewe Huyay,
achana na mimi kwani sitafanya unaloniitia, hakika mimi sijaona kwa
Muhammad ila utekelezaji na ukweli”. Lau ingelikuwepo upande wa waislamu
sababu yo yote iliyowapelekea Baniy Quraydhwah kuwafanyia usaliti huu,
ingeliwastahikia kufanya hivyo.
F
Fakaifa na huu ni
usaliti unaoulipa ukweli na utekelezaji?
F
Fakaifa na huu ni
usaliti uliokusudia kuufyekelea mbali na kuitokomeza kabisa dola ya Kiislamu?
F
Fakaifa usaliti huu
ulikusudia kuingamiza dini ya haki ambayo kwayo Allah amemtumiliza Mtume wake
wa mwisho ili kuzishinda dini zote?
F
Fakaifa na ahadi
iliyokuwa baina yao na Mtume wa Allah iliwataka kuwalinda waislamu na sio
kuwafanyia uhaini na usaliti katika kipindi hiki kigumu kuwahi kuwapitia?
Ukweli
khasa ni kwamba kitendo hiki cha Baniy Quraydhwah hakikuwa ni uvunjaji wa
ahadi tu bali wakati huo huo kilikuwa ni usaliti na uhaini pamoja. Kiasi cha
kuonwa ni kibaya mno hata na watu wao wenyewe walipokuwa wakiujadili ujumbe
ulioletwa kwao na Huyay Ibn Akhtwab, wakasema: “Ikiwa hamtamnusuru Muhammad,
basi muacheni na adui yake”. Zaidi ya yote hayo huo ulikuwa ni usaliti duni
na uhaini wa kipuuzi, kwa sababu huko ni kumchoma kwa nyuma mtu aliyekupa
mgongo huku akikuamini.
II.
Jazaa maumbile juu ya usaliti huu muovu:
Hebu tujiulize nini
huwa malipo ya usaliti na uhaini kama huu katika kanuni/sheria za kimataifa?
Na nini huwa malipo na jazaa ya wahaini na wasaliti hawa katika kivuli cha
dini, haki na uadilifu? Je, ni dhulma kuwapa jazaa inayolingana na uzito wa
matendo yao na kufanyiwa kama walivyokuwa wakitaka kuwafanyia wenziwao? Hapana
shaka kwamba hii ndio jazaa maumbile inayokubaliwa na dini zote, inakubaliwa
na sheria za vita zile za kale na za sasa na inakubaliwa na kila sauti ya haki,
uadilifu na murua. Basi je, baada ya kutendewa yote hayo bado waislamu
watakuwa na hatia wakiwazingira wasaliti hawa mpaka wakajisalimisha mikononi
mwao? Kisha wakawafagia kama wao walivyotaka kuwafagia? Je, bado ilimkinika
waislamu kupata amani kwa upande huu wa Mayahudi baada ya usaliti huu? Je,
waislamu wawaache wasaliti hawa kuendelea kuwa miongoni mwao wakizichuka siri
zao na kuwapelekea maadui zao? Je, ilikuwa ni lazima waislamu kuwafukuza
Madinah wasaliti hawa kama walivyowafukuza Banin- Nadhwiyr hapo kabla?
Wawaachie wakiwa huru katika ardhi wayakusanye makabila na makundi dhidi yao?
Yalikuwa ni maumbile khasa waislamu kujisafisha na wasaliti na wahaini hawa na
wawatendee kama wao walivyotaka kuwatendea.
|