Makala
Mwanzo
Uislamu-Utangulizi
Fiqhi na Sheria 
Akhlaaq-Tabia
Sira ya Mtume
Nasaha za dini
Maswali na Majibu
Uliza Suala la dini
Jiunge na Mtandao

 

  MASWALI NA MAJIBU-Masuala mengine ya Dini  


Masuala mengine ya Dini-Sehemu ya Nne                              
 
  1. Swali langu ni jee kuvaa nguo zenye majina ya watu maarufu au club za mipira inajuzuu?

  2. napenda kuja kwa urefu kuhusu kumuhakikia(HAQIQA)

  3. Nini hukmu ya kukata panki kwa wanaume na kuunganisha nywele.

  4. Nimeona watu wengi wakienda kula katika majumba ( manyumba ) ya wanaohuzunika baada ya kifo ya mwislamu bila hata kuwasaidia kuchimba kaburi au kuswali katika janaza. Je, hii ni halali?. Na kwa nini watu hupika chakula kwa uwingi hata wakafilisika na mwishowe ni wafakiri?

  5. Naomba unijibu kwa saraha suala hili: Mimi ni muhasib kazi yangu kama Muhasib yeyote yule, kazi yangu ni kujenga na kupanga na kuweka hesabu za idara yangu. Kila siku napokea na kuweka, kulipa na kutoa na kusambaza mali (pesa) namna kwa namna sehemu mbali mbali. Kama inavyojulikana kazi hii siku zote kuna kupata na kukosa na mara nyingine kupatwa. Katika kipindi fulani nimeweza kudunduliza pesa kiasi cha mshahara wangu kwa njia ya ziyadat za kila siku zisizo daiwa na wenye kulipa malipo mbali mbali (Unclaimed Payments & Deposits)  Nilitokezewa na shida kali siku moja na kwa kweli nimezitumia kwa hiyo haja yangu, kama niliyokutajia hapa hizi pesa tunaziita "unclaimed Funds" ki-hesabu hizi pesa tunazitia/kwa matumizi ya Petty Cash. Hakuna ubaya wowote, Jee ki-dini,ki-isilamu hizi pesa ni halali au haramu?? hal inabidi sasa nizilipe ikiwa ni haramu? maana ni nyingi na kwa kipindi kikubwa sasa, nishajibiwa majibu mbali mbali lakini sijatosheka, naomba ufafanuzi na jawabu la saraha. Naomba msamaha suala langu nimeliuliza kwa kirefu.

  6. Swali langu naomba kufahamishwa historia sahihi juu ya mama MARYAM BINT IMRAN Inshaallah: Kwamba Je, Yeye baada ya kumzaa ISSA (YESU), Kisha baada ya hapo aliolewa na NANI?. Kibiblia katika mihadhara wasomapo biblia nawasikia wakitamka kutoka katika biblia kwamba Yusufu ndiye aliyekuwa kamchumbia Maryamu, Kisha alipojua kwamba anamimba akaamua kumuacha kwa siri, ndipo malaika akamtokea katika njozi akimwambia Yusufu kwamba "usihofu kumwoa Maryamu Mkeo yeye kabeba mimba kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na mtoto atakayezaliwa jina lake ataitwa Yesu". Sasa Je, huyo Yusufu aliyetajwa pale ndiye yule Nabii Yusufu mtoto wa mzee Yakub aliyekuwa Misri baada ya kutupwa kisimani na ndugu zake au mwingine?
     Naomba nijibiwe kwa mujibu wa historia ya kiislamu kwamba mama Maryamu yeye aliolewa na nani ili nijue ukweli hasa kwa 100%.

  7. Swali ni kuwa nimejaribu kuuliza waislam walio wengi na majawabu yapandana, kuna wanaosema amekufa na kuna wanaosema hajafa Nabii ISSA (A.S) Je niwe na msimamo gani katika ya hayo mawili nauliza.

  8. INATAKIKANA MTU ASOMAPO QURANI AWE NA TWAHARA.SASA KAMA NIPO NA ASIYEJUA UISLAM(MNASWARA)NA ANATAKA MSAHAFU AUSOME NIFANYEJE?

  9. INAJUZU MWANAMKE KUJISAFISHA MIGUU YAKE NA MIKONO KWA KUTOKANA ANAMSAFISHIA MUMEWE.TUNAJUWA KUTOWA NYUSI NI HARAMU.  JE KUTOWA MALAIKA YA MIGUUNI NA MIKONO. NTAOMBA KUPEWA JIBU KUTOKA KWENYE QUR ANI AU HADITH ZA MTUME S.A.W.

  10. ninataka kujua jee kuna hadith yeyote au ushahidi wowote unaokubalisha kufunga na kukithirisha duaa kwenye 15 shabaan?



 

JIBU

 

Rudi Nyuma                                                  Endelea Mbele


| Tuandikie |