Makala
Mwanzo
Uislamu-Utangulizi
Fiqhi na Sheria 
Akhlaaq-Tabia
Sira ya Mtume
Nasaha za dini
Maswali na Majibu
Uliza Suala la dini
Jiunge na Mtandao

 

  MASWALI NA MAJIBU-Ndoa na Talaka  


Ndoa na Talaka-Sehemu ya Kwanza                              
 
  1. Naomba kujua iwapo mwanamke aliye katika eda ya kufiwa na mumewe, je wanaume  ambao sheria inawaruhusu baada ya eda kumuoa wanaruhusiwa kumuona kwa ajili ya kumpa pole nina maana kuonana nao hata kama hawana nia ya kumuoa,asante.

  2. naomba kuuliza kuwa ni (a) haki ya mtoto wakike kuchukuliwa mahari yake nawazazi wake kidini ina uhalali, naomba jibu kwa ushahidi wa qurani au hadithi ya mtume.
    Ikiwa mtu halali na mumewe kwa muda mrefu na anae ndani ya nyumba nini hukumu yake?

  3. je!mtoto wa nje ya ndoa mtoto wa nje ya hali!na baba mkristo na baba muislam atafuata dini ipi katika hizo

  4. kama tunavyojua kwamba ikiwa mwanamke anaachika pindipo mumewe hawezi kazi ya kijamii ( kuingiliana) na mkewe, je! inafaa mwanaume kufunga ndoa na mwanamke tasa (asiezaa kuzaa)? au anaeumwa na maradhi ambayo hayamruhusu kuzaa? naomba ufafanuzi

  5. suali langu liko hapa! ikiwa kila mtu atachagua mke mzuri na wakati sio wanawake wote wazuri, Je! nani ataowa wale wabaya? je uchaguzi huu wa wanawake ni halali?

  6. la kwanza, Je kuna ruhusa yoyote ya kisheria  kwa mwanaume wa kiislam kutumia vijidonge  ambavyo havina madhara  mwilini  ili aongeze nguvu za kiume? na hii inatoka na malalamiko ya mkewe mtu kuwa bwana siku hizi hunifikishi yaani unitoshelezi kama zamani kulikoni? na magomvi haya yanapelekea ndoa kuyumba kwa kila mmoja kuona kuwa mwenzi ameshamchoka, je kuna ruhusa ya kumuona mtaalam Dr ili aandike dawa  ambazo hazitokuwa na madhara ili  amani irudi kwenye nyumba hiyo?
     
    swali la pili
    nini hukumu ya kisheria ya mwanaume amabye amekuwa akimtishia mkewe mara kwa mara inapotokea kuto kuelewana mume hutishia kuandika talaka nakuacha sasa hivi au toka humu ndani, mwanamke amekuwa na heshima ya uoga kwa mumewe kwa kutishiwa talaka, je kuna uhalali wowote wa  mume kumtishia mara  zote mkewe nakuacha huku ameshika peni na karatasi?

  7. Nimefunga ndoa ya kwanza na mke wangu ambayo ilikuwa ya kimila kwa sababu mke wangu alikuwa mkristo baadaye alibadilisha dini na kuamua kufunga ndoa ya kiislamu siku mbili kabla ya mfungo wa ramadhani.

    Swali langu ni kwamba katika ndoa hiyo hakuna hata wazazi waliofika katika ndoa yetu kutoa baraka, si wazazi wa mke wangu wala wazazi wangu? zaidi ya marafiki zangu.Je swali langu nataka kufahamu je kutofika kwa wazazi wa pande mbili katika ndoa hiyo nitakuwa nimepata dhambi kwa mwenyezi mungu

  8. Swali langu la leo ni kuwa; Iwapo kuna mtu aliyeowa kwenye mwaka 1950 kwabahati mbaya hakumaliza mahali ina maana ana deni katika hiyo mahari la shilingi 300/= na leo hii mwaka 2003 anataka kulilipa; JE atalipa ile ile shilingi 300/= au zaidi? asante.

  9. Mimi kuna swala ambalo nigumu sana linanitatanisha kuhusu KITOVU CHA MTOTO-MCHANGA WA KIUME, kwamba eti kitovu chake kitakapomdondikea katika uume wake siku ya kukatika basi asilani uume wake utakuwa haufanyi kazi-kabisa. 
     JE, NI KWELI?? na ikiwa ni kweli. Naomba munijibu na ikiwa kama kuna ushahidi katika Qurani au wa hadithi ya Mtume S.A.W, au utafiti wowote uliyofanyika kuhusu swala hili munifafanulie kwavyo. Nasisi waislamu ni HARAMU kuitikadi mambo ambayo hayana Dalili.

  10. mie mume wangu ni mlevi sana na miye na jitahidi sana kushika dini yangu, nayeye pia namtoleya mawaidha ya deni afahamu lakini bado anadharau na alokuwa ya meharamishwa kwenye dini yeye anataka niyafanye je huo mume ninfate tu maasi kama hayo anasema nifanye kwani wanasema ibada yako unafanya weye mwanamke haikubaliwi mpaka mume wako ufatishe anayoyataka ufanye. kwahisani yenu mnipe shauri yakufanya

JIBU

 

                                                                          Endelea Mbele


| Tuandikie |