Makala
Mwanzo
Uislamu-Utangulizi
Fiqhi na Sheria 
Akhlaaq-Tabia
Sira ya Mtume
Nasaha za dini
Maswali na Majibu
Uliza Suala la dini
Jiunge na Mtandao

 

  MASWALI NA MAJIBU-Ndoa na Talaka  


Ndoa na Talaka-Sehemu ya Pili                              
 
  1. Mimi ninamke wangu wa ndoa, na nimepata nae watoto. Baada ya makubaliano ya kutafuta maisha tukaamua nisafiri niende mbali ya nchi kwa kutafuta maisha ninawashughulikia kwa kila hali na kuwakidhi kimaisha ila tu ni muda mrefu sasa hatujaonana kwa tendo la ndoa. Suala langu:- Baada ya muda kupita mkewangu alinilazimisha kuwa wakati ni mkubwa na hawezi tena kuvumilia ni afadhali nirejee nyumbani kwa kweli hadi hii leo sijapata uwezo wa kurudi.

1.      Jee mwanamke huyu akibeba mimba na kuzaa mtoto jukumu hili litakuwa kwa nani?

2.      Ikiwa atafanya mambo ya zinaa jukumu hili ni kwanani?

3.      Na ikiwa anatoka ndani ya nyumba yake bila amri yangu nani atachukua jukumu hili?

4.      Mwanamke huyu hatokuwa na mchunga kwa muda wote huo jee mimi sitokuwa ni mas-ul juu ya hali hii.

Ninakuomba unitatulie matatizo yangu kuwa hapa ni njia tu nahovia maisha ya baadae.

  1. MARA NYINGI HUTOKEA KUTOELEWANA KWA KUMALIZA EDA YA MWENYE KUFILIWA NA  MUME.SASA VIPI EDA YAKE HUISABIWA KWA MIEZI YA KIISLAMU AU YA KIKRISTO (KIZUNGU)KAMA JAMII ILIVYOZOEA??

  2. MTU ANA MKE WAKE WAMEISHI MIAKA KADHAA GHAFLA MKE AKADAI TALAKA MUME HAKUTAKA KUMUACHA, MKE AKAENDA KWA KADHI NA MUME AKAITWA KWA KADHI, NA BADO MUME AKAGOMA KUTOWA TALAKA KWA MAMLAKA ALIYOPEWA KADHI AKAMUACHA MKE YULE BILA MUME KURIDHIKA NA MKE AKARUDI NYUMBANI KWAO KWA SABABU KESHA ACHWA NA MUME ANASEMA YULE BADO NI MKEWE KWA SABABU HAJAMUACHA, SIKU ZIKAPITA MKE AKAKAA KABLA YA EDA KUMALIZIKA AKABADILI MAWAZO AKATAKA KURUDI KWA MUME WAKE JEE MUME YULE ATAMPOKEA KAMA NI MKEWE KWA SABABU ANASEMA HAJAMUACHA AMA AMREJEE.

  3. swali langu kama mzazi ambaye hajatoka arobaini anaruhusika kuchezeana na mumewe?au si vizuri kufanya hivyo.

  4. kwa nini wanaume wa kiislam wamekubaliwa kuoa wake wanne?

  5. Mimi ni mwanamke wa kislam na nilikutana na mwanamme ambae si mwislam ila baba yake ni mwislam na mamake ni mkiristo na amelelewa katika ukiristo na tumependana nae na tunataka kuishi wote je, kwanza yeye atahesabika ni mwislamu au mkristo? Pili nimemgusia kubadilisha dini amekataa je, itafaa kufunga nae ndoa ya serikali?

  6. JE NDOA INASIHI KUFUNGISHWA NA MWANAMKE AMBAYE YUKO KTKA SIKU ZAKE(HEDHI)?
    NA KAMA INAKUBALIKA VIPI SASA USTAHMILIVU WA MUME KWA MKEWE WAKATI YUKO KTKA  HEDHI NA KWANZA NDIO WAMEOANA?

  7. mimi nimeoa hivi juzi sasa vipi haya madhii huwa yananitoka pasi kutarajia na kwa siku hunilazimu kubadilisha nguo zaidi ya mara moja sasa naona kuwa ni kero je kuna njia nyengine ili niondokane na usumbufu huu ? au ninasamehewa na sheriya kwenda kusali hivyo hivyo??

  8. mimi nina mume nilieozeshwa na wazee wangu, sasa ni miaka mingi hatuna uhusiano wa kindoa lakini tunaishi katika nyumba moja na nishawahi kumwambia ni bora ya kuachana lakini naona hana fikra hiyo, nini ushauri wenu, tafadhali hili linanitatiza sana.

  9. swala langu ni hili nataka kujua katika uislam na ndowa ipo contract ya mume na mke ikiwa mwanamke anataka kuolewa akampa msharti huyo mwanamme nini anataka nini hataki jee inafaa

JIBU

 

Rudi Nyuma                                                  Endelea Mbele


| Tuandikie |