Makala
Mwanzo
Uislamu-Utangulizi
Fiqhi na Sheria 
Akhlaaq-Tabia
Sira ya Mtume
Nasaha za dini
Maswali na Majibu
Uliza Suala la dini
Jiunge na Mtandao

 

  MASWALI NA MAJIBU-Swala  


Swala-Sehemu ya Kwanza                              
 
  1. mimi ni mkazi wa muda mrefu nje ya nchi yangu na nitakuwa hapa kwa muda kiasi takriban miaka mitano au zaidi kidogo, sasa je nini fatwa ya mimi kuswali swala zangu kama msafiri? na maanisha je kuna ruhusa ya mimi kuziswali swala zangu kama msafiri kwa muda wote nitakao kuwa hapa?
    Na je  ni vipi basi nitaziunganisha kama kuna  ruhusa hiyo? na je kama inapatikana fulsa ya mimi kukamilisaha tano kwa kujihisi upungufu fulani kwani kufanya vile usivyozoea inakuwa taabu kwa siku za mwanzoni , je  inaruhusiwa baadhi ya siku kuswali tano kwa wakati hata kama ni utaratibu wangu kuzichanganya kama msafiri?

  2. IKIWA MIMI NIMEZALIWA  ZANZIBAR NA NIMEJENGA ZANZIBAR LAKINI SIISHI NNAISHI OMAN, NA NIMEJENGA NYUMBA OMAN NA NDIKO NNAKO ISHI JE IKIWA NTAKWENDA ZANZIBAR KUTEMBEA NITASWALI WATAN AU SAFAR?

  3. Mimi nauliza kuhusu suala la isibali yaani kuburuza suruali,je ni kweli kuwa yeyote aswalie hali ya kuwa suruali au kanzu inaburuzika swala yake ina mushkeli?Naomba sana jibu liwe na ushahidi ili niweze kuielimisha familia yangu

  4. naomba kujuwa hukmu ya swala ya ijumaa.kwanza iko kwenye kundi gani nifardhi ain kifaya ama sunna.kisha hukmu ya mwenye kuacha ijumaa bila ya sababu ni nini.

  5. Eti baada ya kusali swala yoyote ya faradhi, kisha baada ya kutoa salamu
    ni kharamu kumpa muislamu mwenzio mkono kwasababu: (eti hii ilikuwa ni mila ya wayahudi kunamtu wao alikuwa na kidole gumba gutu cha mkono wa kulia kwahiyo wao walikuwa wakifanya hivyo ili kuitikadi kwamba wapate baraka kutoka kwake!)

    Eti baada ya kusali si vyema kuomba dua kwa pamoja kwasababu kila mtu anamatatizo yake binafsi!.

  6. Huwa napataga safari ya kutoka DSM kwenda TABORA kwa usafiri wa TRENI kwa muda wa mchana-mzima na usiku-mzima hadi saa 4:00 usiku ndio nafika nyumbani
    (i.)Ndani ya treni hakuna maji ili nichukuwe udhu (Je, nifanyeje?).
     
    (ii.)Vile vile pakusalia hakuna, hata kama nikiamua kusali kwa ishara (ikiwa udhu nitakuwa nao) kutokana na ghasia, msongamano, mara mtu anakuomba kwamba simama kidogo ili nichue au niweke kitufulani chini ya kiti; na Mfano wa kama hayo. (Je, nitasali vipi?)
     
    (iii.)Na hili swala la kwamba ukiwa safarini waweza kupunguza SALA zenye rakaa 4 ukasali 2, na waweza kusali kwa pamoja Adhuhuri na Alasiri kutokana na ile misukosuko ya ugenini (Je, jambo hili nikweli kwa ushahidi?)
     
    (iv.)Na katika Swala la kutengukwa na udhu kuna kipengere cha kwamba "Ukigusana ngozi kwa ngozi na mwanamke unaeweza kumuoa kisheria udhu wako unatenguka" Sasa je, kwa hali hii utafanyaje ikiwa unao udhu kisha ukapanda kipando au basi-tauni ukielekea msikiti wa ijumaa halafu ikatokea kugusana na mwanamke, na baada ya kufika huko maji hakuna.?
     
    (v.)Kwa mtu aliyeko mahabusu (Je, Ata Sali vipi na ni mahala pachafu?, Atapata wapi udhu?


  7. je,nikiswali nyuma ya imamu mshirikina(yaani mpiga ramli)swala yangu itasihi?
    pili:    je,nikiingia msikitini kusali sala ya ijumaa hali ya kuwa nimechelewa rakaa zote mbili lakini nimemkuta imam kwenye tahiyatu,je nitanuia kuswali jumaa au dhuhuri?
    mwisho:      naomba ufafanuzu juu ya sala yenye tahiatu nne.(yaani mfano mtu kamuwahi imam kwenye tahiatu ya kwanza kwenye sala ya magharibi akaa kisha tahiatu ya mwisho kwa imam nae akakaa kisha imam alipotoa salamu kwake ikawa ndio kwanza kamaliza rakaa moja hivyo baada ya kunyanyuka akasali rakaa ya pili akakaa tahiatu kisha akanyanyuka na kumaliza rakaa ya mwisho akakaa tahiatu ya mwisho)
    kama nimeeleweka vizuri itakuwa huyu mtu kakaa tahiatu nne.je sala hii haitakuwa na dosari yoyote?

  8. Mtume wetu ametusisitiza sana juu ya kusali msikitini kwa wanaume.
    je mwanaume anaruhusiwa kusali nyumbani ikiwa anaogopa akitoka kwenda msikitini pengine waizi watavunja nyumba yake na kuiba?au pengine ni sala ya asubuhi nae anaogopa pengine atavamiwa na majambazi au labda anaweza kuumwa na mbwa?


  9. Katika kufunga mikono katika sala naona kila mmoja anafunga vyake
    atakavyo,yaani kuna wanaofunga chini ya tumbo,kuna wanafunga tumb
    oni,na pia kuna wanaofunga chini yamaziwa,pia kuna wafunga juu ya
    kifua,na kuna wanio achia kabisa hawafungi,mimi nataka ufafanuzi
    kuhusu jambo hili,yaani ipi iliokuwa SAHIHI.

  10. 1)Iwapo nitakuwa kazini mchana hadi jioni na swala ya Alaasir ikanipita nikifika ni magharib jee nitaswali magharib ndio nilipe ya alasir au nitaswali Magharib kwanza kwani ndio muda au muadhini wa magharib ameshaadhini?Naomba ufafanuzi wako!
    2)Jee Inawezekana wakati naswali adhuhuri nikaswali swala ya alasiri kama swala ya safari!Kwa sababu muda wote wa alasir ninakuwa kazini na hakuna mahala ambapo naweza kujihifadhi nikaswali swala hiyo ya alasir1

 

JIBU

 

                                                                          Endelea Mbele


| Tuandikie |